Kenya yasimamisha safari za ndege kutoka kaskazini mwa italia

Serikali
ya Kenya imesimamisha safari za ndege kutoka Kaskazini mwa Italia
kutokana na mlipuko wa nimonia ya COVID-19 nchini humo.


Mwenyekiti
wa Kamati ya kitaifa ya mwitikio wa dharura dhidi ya COVID-19 Bw.
Mutahi Kagwe, amesema safari za ndege kutoka Kaskazini mwa Italia, hasa
miji ya Verona na Milan, kwenda mkoa wa pwani nchini Kenya
zimesimamishwa kuanzia tarehe 3 mwezi Machi.

Bw.
Kagwe ambaye pia ni waziri wa afya wa Kenya amesema, Kenya itaendelea
kufuatilia hali ya nchini Italia na kurekebisha sera yake kulingana na
maendeleo ya hali.