JESHI la Polisi mkoa wa Iringa limetaka jamii kuachakutoa taarifa za upotoshaji juu ya kifo Cha mfungwa Martin Chacha Mwita aliyekuwa amehukumiwa kifungo Cha miezi jela kwa kosa la Wizi wa mafuta diesel Lita 383 katika Kampuni ya Trans Fuel Logistics Ltd
Akizungumza na Waandishi wa habari leo jumamosi March 2/2024 kamishna Msaidizi mwandamizi wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa Allan Bukumbi alisema kuwa February 28 mwaka huu jeshi la Polisi lilipokea taarifa Toka kwa mkuu wa gereza la Iringa kuhusu kifo Cha mfungwa huyo mwenye namba 47/2024 Martin Mwita Chacha (46) mkazi wa kunduchi Dar es Salaam.
Alisema Chacha alikuwa dereva katika Kampuni Trans Fuel Logistics Ltd ya ambapo alikuwa akitumikia kifungo Cha miezi mitatu jela katika gereza la Iringa tangu February 20 mwaka huu baada ya kupatikana na hatia kwa kosa la Wizi wa mafuta jinai namba 62/2024 iliyotolewa na hukumu na mahakama ya Mwanzo Iringa mjini .
“Marehemu Chacha alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa baada ya kuugua ghafla alipopatwa na Maumivu makali upande wa moyo na kulalamika kwa wafungwa wenzake waliokuwa nae kwenye shughuli za Kilimo eneo la gereza la Mlolo na kukimbizwa Hospital haraka” alisema RPC Bukumbi .
Kuwa mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa uchunguzi zaidi wa kitaalam ili kubaini kifo chake Marehemu kilisababishwa na nini japo taarifa za awali za daktari zinaonesha kuwa Marehemu alikuwa na tatizo la ugonjwa wa moyo .
“Mwili haujafanyiwa uchunguzi (Postmoterm) na ni Hatari Sana kwa kuanza kutoa taarifa ambazo hazijafanyiwa uchunguzi wa kitaalam na kudai kuwa ameuwawa kwa kipigo ,uchunguzi utafanyika na jeshi la Polisi linatoa wito kwa yeyote mwenye Ukweli wowote wa kuweza kukamilisha uchunguzi na kupata ushahidi madhubuti asisite kujitokeza”
Pia alisema jeshi la Polisi linatoa Rai kwa Wananchi kujiepusha na utoaji wa taarifa za uongo na upotoshaji badala yake kusimama kwenye Ukweli na Si mambo ya kuzusha kwa malengo ambayo hayatasaidia watanzania .