Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema aliyekuwa Waziri wa Ardhi William Lukuvi hatagombea Uspika wa Bunge bali amemsogeza Ikulu ili amsaidie kazi zake Ikulu huku Palamagamba Kabudi naye akipewa kazi maalumu Ikulu.
“Kaka yangu Lukuvi, yeye ana kazi na mimi, mtaisikia baadaye. Lakini namvuta Ikulu, kazi yetu ni kuwasimamia nyinyi.Hatagombea Uspika”- Rais Samia
“Kabudi amefanya kazi nzuri sana kusimamia majadiliano ya serikali na mashirika, na ndiyo kazi ninayotaka nimkabidhi sasa kindakindaki…Mashirika yote, kazi zote zitakazoingia ubia na serikali, Kabudi ataongoza hiyo timu. Kwa hiyo yeye ni baba mikataba.”- Rais Samia