Na Joyce Joliga
Tunduru.
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru, wametakiwa kushiriki kwenye zoezi la utoaji wa elimu ya kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu na kusimamia malezi na makuzi ya watoto wenye mri wa miaka 0-8 hasa kipindi cha ukuaji ili kuwa na taifa bora na kusaidia watoto kupata elimu na kutimiza ndoto zao.
Hayo yamesemwa na Ofisa maendeleo ya jamii mkoa Mariam Juma wakati akitambulisha program ya Malezi na makuzi ya Mtoto kwa Madiwani wa Halmashauri hiyo kwa niaba ya Ofisa Ustawi wa jamii wa mkoa wa Ruvuma Victor Nyenza.
Program ya malezi na makuzi na maendeleo ya Mtoto imetambulishwa jana kwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru katika kikao Cha Baraza la kawaida la robo ya pili ya mwaka wa fedha 2024/3015 kilichofanyika katika ukumbi wa klasta ya walimu wa taarifa ya mlingoti mjini .
Mariam alisema , serikali imeagiza jamii kuwekeza zaidi kwenye malezi bora kwa watoto chini ya miaka 0 hadi 8 kipindi ambacho ubongo wa mtoto hukua kwa asilimia 100 na kuwa muongozo wa maisha yake yote
Aidha,Madiwani wametakiwa kuiingiza program hiyo kwenye mipango yao ya Halmashsuri kwa kuungiza kwenye bajeti zao ili utekelezaji wake uweendelevu.
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wakifatilia uzinduzi wa program ya malezi na makuzi ya Mtoto wakati wa kikao cha baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo . |
Alisema ingawa matokeo ya mpango huo hayawezi kuonekana kwa haraka lakini juhudi zake zinalenga kuwalea watoto kwa kufuatia misingi imara ya maisha Bora kwa kuwa na faida kubwa kwa taifa .
Alisema katika utekelezaji huo serikali imewaelekeza maafisa ustawi wa jamii , maafisa kutoka Idara ya maendeleo ya jamii maafisa wa madawati ya jinsia pamoja na NGOs kushiriki kwenye utowaji wa elimu hiyo.
Akizungumzia program hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Haillu Hemedi Mussa alisema kuwa taarifa hizo zimefika kwa wakati na kwamba Halmashauri yake imeipokea kwa mikono miwili na akaahidi kuifanyia kazi
Alisema program hiyo kwa wilaya ya Tunduru ni muhimu kutokana na wilaya yake kuwa nyuma kwa elimu na kwamba ufuatiliaji wa malezi hayo utawasaidia wananchi kuwa na watoto Bora .
Naye Benaya Wilishangi, anawataka madiwani kusikiliza wataalam wa mezi na makuzi ili kujenga jamii yenye ustawi bora ikiwa ni pamoja na kuondokanana udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano.