Na Mwandishi Wetu Mara.
Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Musoma Mkoani Mara imeendelea kusikiliza kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara Lucas Sotel kwa mara ya pili ambapo hii leo mashahidi wawili wametoa ushahidi wao katika mahakama hiyo inayoendelea wilayani Tarime Mkoani Mara.
Lucas Sotel anakabiliwa na kesi ya Mauaji ya kijana Wankuru Nyamhanga Mkazi wa kijiji cha Buriba Wilayani Tarime Mkoani Mara mauaji anayodaiwa kuyatenda Agosti 04 Mwaka 2014.
Akitoa ushahidi mahakamani hapo shahidi wa kwanza Bernard Makonyo ambaye ni daktari wa binadamu alisema kuwa Novemba 11 mwaka 2014 akiwa kazini katika Hospitali ya wilaya ya Tarime akiwa mganga mfawidhi wa hospitali hiyo akiwa na ndugu wa marehemu na askari wa jeshi la polisi kituo cha Sirari alifanyia uchunguzi mwili wa marehemu nakubaini alikuwa na jeraha lililosababishwa na kitu chenye Ncha kali jambo ambalo lilisababisha kuvunja kwa damu nyingi na kusababisha kifo cha Marehemu Wankuru.
Akitoa Ushahidi katika mahakama hiyo Shahidi wa pili ambaye ni Askari Polisi kitengo cha upelelezi kituo cha polisi Kinesi Koplo , Mustapher ambapo kipindi tukio hilo linatokea askari huyo alikuwa kitengo cha Upelelezi kituo cha polisi Sirari.
Askari aliiambia mahakama kuwa alipokea jalada linalohusiana na taarifa za kifo Wankuru taarifa ambazo zilitolewa na mwenyekiti wa kijiji cha Buriba kuwa alipigiwa simu na mlinzi wa mnara wa aitel uliopo kijiji cha Buriba kuwa kuna mwili wa marehemu ndipo walienda eneo la tukio ambapo aliongeza kusema kuwa walikuta mawe pembezoni ,wa barabara na ndipo walitoa mwili nakupeleka Hospitali ya wilaya ya Tarime kwa ajili ya uchunguzi nakurejea eneo la tukio kwa ajili ya kupima juu ya tukio hilo.
Upande wa Jamhuri unaowakilishwa na Yesse Temba uliomba Mahakama hiyo kupokea vielelezo viwili mahakamani hapo kama ushaidi kikiwemo kelelezo cha uchunguzi wa Mwili wa Marehemu pamoja na ramani iliyochorwa katika eneo la tukio hilo la mauaji ya kijana Wankuru na mahakama ilikubali ombi hilo na kesi kuendelea kusikilizwa.
Wakili upande wa Serikali Yese Temba aliomba Mahakama kufunga kesi ya awali baada ya mashahidi wanne kutoa ushahidi wao na mahakama kupokea vielelezo viwili kama ushahidi na ndipo Mh: Jaji alifunga kesi ya awali na kuahirisha kesi hiyo kwa muda.
Baada ya mahakama kurejea Mshitakiwa Lucas Sotel alijitetea mahakamani hapo ambapo alidai kuwa katika kesi hiyo atakuwa na shahidi mmoja.
Sotel aliambia Mahakama kuwa kipindi anatoka Sirari majira ya saa4 usiku akiwa na rafiki yake aliyejulikana kwa jina la Msabi Magasi walipofika eneo la Buriba nakukuta mawe yameziba barabarani ndipo walishuka ili kutoa mawe hayo kundi la vijana lilitokea nakuwambia wakae chini ndipo alifyatua risasi moja juu na kundi hilo kutawanyika.
Baada ya kufyatua risasi hiyo waliendelea kutoa mawe na ndipo kundi hilo lilitokea kwa mara nyingine na kufyatua risasi ya pili na kundi hilo kutawanyika walipofanikiwa kutoa mawe hayo walielekea nyumbani kwake na Msabi na baadae Sotel kuelekea Nyumbani kwake.
Upande wa Utetezi kupitia kwa wakili Selina Magoiga waliomba mahakama hiyo kufunga kesi upande wa utetezi ambapo Mh Jaji John Kahyoza alifunga ushahidi na kuiambia mahama kuwa kilichobaki kusikilizwa ni hoja za Mwisho na ndipo aliharisha kesi hiyo ambapo itasikilizwa tena hapo leo Novembe 30 majira ya Mchana.