Sekretariet ya Chama Cha Mkoa wa Morogoro ikiongozwa na Katibu wa CCM mkoa Shaka Hamdu Shaka wameendelea na ziara ya kukutana na Secretariet za kata zote 214 mkoa wa huo
Ziara hiyo ya kawaida kuhimiza uhai wa Chama pamoja na kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa ngazi ya kata wa Chama na jumuiya zake.
Mafunzo hayo yanaendeshwa na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM Ndugu Ruta yameendelea wilaya ya Mvomero na Morogoro Mjini zilizojumuisha sekretariet za kata 59.
Aidha Katibu wa CCM mkoa amezindua rasmi mpango mkakati wa mkoa wenye kauli mbiu ya “MAJIRANI WAMCHAGUE JIRANI MWENZAO ANAETOKANA NA CCM” ambao utakwenda kusimamiwa na sekretariet za kata katika utekelezaji wake kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa vijiji na vitongoji