Marekani yapanga kuwahamisha wanajeshi wake 11900 kutoka ujerumani

Marekani inapanga kuwahamisha wanajeshi wake 11,900 kutoka Ujerumani, kufikia wanajeshi 24,000 kutoka jumla ya wanajeshi 36,000, wengi kuliko ilivyotangazwa hapo kabla, waziri wa ulinzi wa Marekani mark Esper amesema hayo jana
Esper amewaambia waandishi habari leo kuwa karibu wanajeshi 5,600 watahamishiwa katika mataifa mengine ya jumuiya ya NATO, wakati 6,400 watarejea nchini Marekani, ambapo wengi watabadilishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine katika bara la Ulaya.
Ameongeza kuwa hatua hiyo inafanyika, katika hali ambayo itaimarisha jumuiya ya NATO, kuimarisha vizuwizi dhidi ya Urusi, kutoa hakikisho kwa washirika na kuimarisha uwezo wa Marekani kuchukua hatua za kimkakati.
Rais Trump alitangaza mwezi Juni mipango ya kuwaondoa kwa kiasi fulani wanajeshi wa Marekani huku kukiwa na mvutano wa muda mrefu na Ujerumani kuhusiana na matumizi katika ulinzi.