Masoko ya hisa duniani na masoko ya hisa nchini Marekani yameporomoka leo baada ya hazina ya Marekani kuonya kwamba janga la virusi vya corona huenda likatishia hali bora kidogo iliyojitokeza ya uchumi kurejea katika hali ya kawaida na kuweka viwango vya riba karibu ya sifuri.
Kuanguka kwa hisa kulikoongezwa kasi katika mataifa ya Ulaya baada ya Ujerumani kusema uchumi wake ulinywea kwa asilimia 10 katika robo ya pili kutoka kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
Data za pato jumla la taifa nchini Marekani zinatarajiwa kutolewa baadaye leo, wakati hesabu za jumla kwa upande wa mataifa ya bara la Ulaya zitatolewa kesho Ijumaa.
Viwango vya chini vya riba na matarajio ya wawekezaji juu ya uwezekano wa kupatikana chanjo vimesaidia masoko ya dunia kurejea katika hali nzuri katika sehemu kubwa ya mwaka huu.