Mbio za nmb kufanyika septemba 24, dar es salaam

 Wakimbiaji 6000 kushiriki mbio za NMB September 24

Jijini Dar es salam

Na Queen Lema Arusha 

Wakimbiaji zaidi ya 6000 kutoka ndani na nje ya Nchi wanatarajiwa kushiriki mbio za hisani za NMB marathon zinazotarajiwa kufanyika September 24 mwaka huu jijini Dar-es-Salaam.

Aidha Mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika katika viwanja vya leader’s club zenye kauli mbiu ya ‘NMB sambaza upendo’ zinalenga kukusanya kiasi Cha shilingi milioni 600 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya wanawake wenye Fistula kote nchini.

Akiongea na  waandishi wa habari mkoani Arusha, Meneja wa NMB banki tawi la Arusha, Emmanuel Kishosha alisema kutokana na umuhimu wa mbio hizo wamewapa kazi wanariadha wa kimataifa kutoka Tanzania, Kuzitangaza mbio hizo.

“Sisi kama Nmb tumeletea  mwanariadha kama  Emmanuel Giniki na Gabriel Geay pia Failuna Matanga kuwa wahamasishaji wa mbio zetu ili tuweze kutimiza lengo la kuwasaidia wanawake wengi wenye fistula nchini” alisema 

” wanariadha 6000 watashiriki mbio zetu, kutoka ndani na nje ya nchi ili kufanikisha kukusanya kiasi Cha shilingi milioni 600 tutakazokabidhi katika hospital ya CCBRT zikatumike kutibu ugonjwa wa Fistula ambao umekuwa ukiwasumbua wamama”

Alisema kuwa maandalizi yote kuelekea mbio hizo zimekamilika na washiriki wanaendelea kujisajili katika vituo vyao kwa gharama ya shilingi 30,000 kwa kilomita 21, huku kilomita tano na 10 wakijisajili kwa shilingi 20,000 na kupatiwa vifaa vya ushiriki ikiwemo namba na fulana.

Wakizungumzia ushiriki wao, wanariadha hao walisema kuwa watashiriki umbali wa kilomita 21, ili kutoa mchango wao kwa wanawake waathirika na fistula wapatiwe matibabu bure.

“Niombe wanariadha wenzangu na wakimbiaji wote nchini wajisajili kushiriki mbio hizi za hisani ili kuwaokoa dada na mama zetu waliokumbwa na ugonjwa wa Fistula na hii itakuwa Kama sadaka Safi na hazina katika maisha yetu