Meya ngwada ampongeza mnec asas kwa kuchangia madawati 5000

Mstahiki meya wa  Manispaa ya Iringa Ibrahim Gwada amempongeza mkurugenzi wa kampuni ya Asas Salim Abri Asas kwa kuchangia madawati 500 kwa shule zenye uhitaji zilizojengwa kwa ajili ya wanafunzi watakao anza kidato cha kwanza mwaka huu.Mwandishi Raymond Minja anaripoti 

Akizungumza wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Iringa Ngwada alisema kuwa mkurungenzi wa kampuni ya Asas Salim Abri Asas amejitolea madawati 500 katika Shule mpya zenye uhaba wa madawati ili kusaidia kupunguza changamoto ya madawati

Alisema kuwa mkurugenzi huyo wa kampuni ya Asas amekuwa mdau mkubwa wa naendeleo  kwani amekuwa akijitoa sana kwenye kuchangia shunguli mbalimbali za maendeleo,

“Naomba kuchua nafasi hii kumpongeza ndugu Salim Abri Asas kwa juhudi zake ambazo amekuwa akichangia katika maendeleo katika maeneo ambayo wanahitaji msaada bila ni mdau wetu mkubwa Sana’a”

Ngwada alisema kuwa madawati hayo 500  yatasaidia kupunguza uhaba wa madawati katika shule zilizopo manispaa ya Iringa hivyo mkurugenzi wa kampuni hiyoameipinguzia mzigo  halinashauri hiyo

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi alishukuru juhudi zinazofanywa na  kampuni ya Asas  kwa kazi kubwa anazozifanya za kimaendeleo mkoani Iringa .

Hata hivyo mkuuu wa alimtaka afisa  elimu kukaa na wakuu wa Shule za binafsi na za serikali ili kupunguza adha ya wanafunzi kubeba mabegi yenye uzito mkubwa pamoja na kupata muda wa kujisomea  masomo ya jioni