Mkurugenzi mkuu wa EWURA Mhandisi Modestus Lumato katikati akiwa na wadau na wafanyakazi wa EWURA alipotembelea viwanja vya maonesho ya utalii ya karibu kusini katika eneo la Kihesa Kilolo mjini Iringa leo
Mkurugenzi. Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Mhandisi Modestus Martin Lumato amesema jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassa katika ukuzaji wa uchumi wa Taifa kupitia sekta ya utalii ni kubwa sana na wao kama EWURA wanaendelea kuunga mkono jitihada hizo kwa kuhakikisha wanasimamia vema huduma za Nishati na maji kuona hakuna uchakachuaji .
Akizungumza leo baada ya kutembelea banda la EWURA katika maonesha ya utalii ya Karibu kusini katika viwanja za Kihesa Kilolo mjini Iringa Mhandisi Lumato alisema kuwa kila mmoja ni shahidi kwa kazi nzuri na kubwa inayofanywa na mheshimiwa Rais Samia katika kutangaza utalii kupitia filam ya The Royal Tour ambayo imeweza kutangaza utalii Dunia nzima .
Kwani alisema kuwa wakati Rais Samia akifanya jitihada kubwa za kutangaza utalii ngazi ya kimataifa mikoa nayo imeendelea kuunga mkono jitihada hizo kama ambavyo mikoa 10 ya kusini na nyanda za juu kusini ilivyoweza kuandaa maonesho hayo kwa ajili ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo mikoa ya kusini na nyanda za juu kusini .
Alisema mkakati huo ni mzuri na utasaidia kuhamasisha jamii kupenda kutembelea vivutio vya utalii pia kuendelea kufungua milango kwa wageni kutembelea hifadhi mbali mbali nchini na kukuza uchumi wa Taifa .
Mhandisi Lumato alisema wao kama EWURA kwa kuunga mkono maonesho ya utalii ya karibu kusini wamechangia kiasi cha Tsh milioni 10 pamoja na kuungana na uongozi wa mkoa wa Iringa na mikoa mbali mbali kwenda kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha .
” Sisi EWURA tumeona ni juhudi nzuri katika kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita katika kutangaza utalii na wote ambao watakwenda kutalii Hifadhi ya Ruaha baada ya kurejea itakuwa ni mwanzo wa kuendelea kueneza elimu ya utalii wa ndani ndani ya familia na nje ya familia zao”
Alisema kuwa sekta ya utalii imekuwa zaidi katika mikoa ya kasikazin ila kutokana na jitihada za serikali kutangaza utalii nje itasaidia zaidi milango ya utalii kwa mikoa ya kusini kuongezeka zaidi.
Mhandisi Lumato alisema kuwa EWURA wamekuwa sehemu ya utalii kutokana na wateja wao ni watumiaji wa Nishati na maji hivyo kupitia maonesho hayo wataweza kutoa elimu mbali mbali kwa wananchi pamoja na kupokea malalamiko yao kwa wateja wa huduma za umeme na Maji .
Aidha alisema EWURA katika kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora wataendelea kuchunguza ubora wa mafuta pamoja na bei zao na kuona vituo vya kuuza mafuta vinakuwa bora zaidi na sio bora vituo .
Kwa upande wao wananchi waliotembelea banda la EWURA wamepongeza jitihada za EWURA katika kusimamia ubora wa Nishati na Maji na kuwa wanaomba huduma hiyo ya elimu kwa umma kuendelea zaidi .
Banda la EWURA katika viwanja vya maonesho ya utalii karibu kusini
Mkurugenzi mkuu wa EWURA Mhandisi Modestus Lumato akiwa katika banda la Tanesco