Bondia wa kimataifa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo amesema watu wengi hawaujui vyema mchezo wa ngumi ndio maana wanaongea vitu ambavyo awavifahamu.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Mwakinyo ameandika ujumbe unaosomeka.
“Watu wengine hawajui tu nini maana ya ndondi vitu ambavyo watu husema wakati mwingine hunifanya nifikiri kuwa bado wanahitaji kujifunza kuelewa polepole” alisema Mwakinyo.