Mwandishi afikishwa mahakamani kwa kosa la kuchapisha habari ya uongo facebook ,apelekwa mahabusu


Mwandishi
wa  habari wa kujitegemea   anayeandika  habari  zake  katika ukurasa 
wa kitabu sura (face Book )katika  wilaya ya Mufindi  mkoa wa  Iringa 
Sebastian Atilio  amefikishwa  mbele ya  hakimu  mkazi  wa mahakama ya 
 wilaya ya  Mufindi kwa  makosa mawili  likiwemo la kuandika habari za
uongo na  kufanya kazi  bila  kusajiliwa na bodi  anaripoti mwandishi
Francis Godwin kutoka mkoani Iringa .

Akisoma 
mashtaka  haya  leo   mbele ya hakimu  mkazi wa mahakama  hiyo  Edward 
Uforo, mwendesha mashitaka wa jamhuri Victor  Kitamale  alisema  kuwa 
Sebastian  anashtakiwa  kwa  kosa la kwanza la kufanya kazi  bila 
kusajiliwa  katika  bodi ya  uandishi na  kosa la  pili ni  kuandika
habari za uongo  juu ya  wananchi wa  kijiji cha Ifupila  kuhamishwa .
Hata 
 hivyo msitakiwa   huyo alikana mashitaka  yote yanayomkabili  huku 
mahakama  hiyo  ikisema  kuwa makosa  hayo  kisheria  yanadhamana  .
Wakati 
mwendesha  mashtaka  wa Jamhuri  alipinga  dhamana  hiyo chini ya 
kifungu namba 148(5) D)  cha sheria  na mwenendo wa makosa ya jinai
(sura 20) ambapo  jamhuri  imefaili  kiapo cha kuzuia dhamana  kutolewa .
Huku
upande wa mashtaka  umepewa na mahakama hiyo    nafasi ya  kufaili
hati  kinzani  Septemba 16  mwaka huu   ili Septemba  18  mwaka huu 
maombi ya kutolewa ama  kutotolewa kwa dhamana  yatajulikana .
Wakili 
 wa mwanahabari  huyo Emmanuel  Chengula kutoka  mtandao wa  watetezi
wa haki za binadamu (THRDC)  alisema kuwa  hatua ya kufikishwa
mahakamani kwa mteja  wake ni mwanzo wa haki yake  kupatikana  kwani
polisi  walikuwa  wakimzuia  mahabusu mteja  wao toka  jumamosi 
iliyopita  bila  kumpeleka mahakamani.
 Wakili 
Chengula  alisema  katika  kesi hiyo  kuna maombi ya  kuzuia  dhamana 
ambayo ni  maombi namba 10/2019 na kesi  yenyewe   ya  msingi ni kesi 
namba 208/2019.
Mshitakiwa   huyo amepelekwa katika
mahabusu ya Isupilo  Mufindi hadi   septemba  18  atakapofikishwa 
mahakamani hapo tena kwa ajili ya  kusikiliza maamuzi ya dhamana  yake.