Mkurugenzi wa Taasisi ya chemchem Nicolas Negri Akizungumza katika mchezo wa fainali na kupongeza washindi chemchem cup 2021 |
Wachezaji wa timu ya maklayoni wakifurahia kombe la ubingwa chem chem cup 2021 |
Mwandishi wetu,Babati
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo , Paulina Gekul amekabidhi zawadi Kwa mabingwa wa michuano ya Chemchem CUP 2021 huku akiwataka wanamichezo mkoa Manyara, kuanza kujiandaa na michuano ya Taifa CUP .
Akizungumza mara baada ya mchezo wafainali ya chemchem CUP 2021,katika eneo la Mdori wilayani Babati,Naibu Waziri huyo, amepongeza waandaji ya mashindano hayo kwa kuwezesha kuibuliwa vipaji katika soka
Gekul amesema mkoa wa Manyara, una vijana wengi wenye vipaji vya soka, lakini wanaojulikana ni wa riadha tu hivyo sasa muhimu maafisa ichezo kila wilaya kuandaa timu bora za soka.
“leo nimefurahi kuja katika Fainali ya michuano hii ya Chemchem ambayo imeanzishwa na mwekezaji katika eneo hili ilikutunza mazingira na kuhifadhi wanyama pori na nimeona vipaji vingi sasa tujiandae kwa Taifa CUP”alisema
Naibu Waziri Gekul alikabidhi kombe kwa timu ya Maklayoni mabingwa chemchem CUP 2021 na fedha taslimu sh 800,000,baada ya kuichapa timu ya Minjingu FC magoli 4-1, ambayo nayo ilipata kombe na fedha taslimu sh 500,000.
Timu ya Gembea Fc ilikabidhiwa fedha taslimu sh 300,000 kwa kuwa timu ya tatu,huku timu ya Ashapopo akipokea zawadi ya sh 100,000 kuwa timu ya nidhamu,Kocha bora Pepe Samweli wa Minjinfu FC alipata 50,000.
Katika michuano ambayo timu zote 10 zilipewa jezi na mpira ,mfungaji bora Hamfrey Alex wa Maklayoni Fc 50,000 Amri Yote alikuwa mchezaji bora kutoka Macedonia aliyezawadiwa 50,000 na kipa bora alishinda Saidi Hamis wa Mdori FC.
Awali Mkurugenzi wa kampuni ya chemchem ambayo imewekeza katika eneo hilo la hifadhi ya jamii ya BURUNGE, Nicolaus Negri alisema michuano hiyo tangu imeanzishwa imekuwa na mafanikio na tayari imetoa wachezaji ambao sasa wanashiriki ligi kuu ya NBC.
“licha michuano hii kutumika kupingavita ujangili, kutunza mazingira na kuendeleza uhifadhi na Utalii lakini hapa kua vipaji na ndio sababu tunatoa fedha kuendeleza michuano hii kila mwaka”alisema
Katibu wa michuano hiyo, John Bura amesema michuano ya chemchem mwaka 2021 imetumia kiasi cha sh 25 milioni, ambapo timu 10 zilishiriki kutokana katika vijiji ambavyo vinaunda hifadhi ya jamii ya Burunge.
Meneja wa miradi wa taasisi ya chemchem fondation ambao ndio wadhamini wa ligi hiyo, Peter Millangwa alisema lengo la kuandaa michuano hiyo ni kuwashirikisha vijana katika uhifadhi na kupiga vita ujangili.
Timu nyingine zilizoshirii michuano hii ni pamoja na Olasiti FC,,Mdori Fc,Mshikemshike FC,Macedonia FC, Youngboys, Star Boys,Gembwe na Sangaiwe .