Naibu waziri aziagiza taasisi za uhifadhi kuunda vikosi maalum kudhibiti wanyamapori

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa na Mkuu wa wilaya ya Lindi, Mhe. Shaibu Mgenda akizungumza na baadhi ya watumishi wakati alipofika katika eneo la kupumzikia watalii katika Msitu wa mazingira asilia wa Rondo ikiwa ni ziara yake ya kikazi ya kutembelea msitu huo kwa ajili ya kutatua changamoto zinazowakabili watumishi pamoja na wananchi wanaoishi karibu na Hifadhi hiyo iliyopo katika wilaya ya Lindi mkoani Lindi. Wa kwanza kushoto mbele ni Mkuu wa HIfadhi ya Rondo, Richard Tarimo
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa kwenye mti wa Mwl. Julius Nyerere ambapo miaka ya 1970 alipofika katika katika kijiji cha Rondo hilo aliomba apelekwe katika eneo unakopatikana mti huo ambapo baada ya kufika alichukua gome la mti huo uitwao Mkufi na kisha akaondoka na gome ;a mti huo licha ya kuwa haijulikani alikwenda kulifafanyia nini gome hilo la mti huo ambao umekuwa kivutio kikubwa cha utalii na watu wengi kutoka maeneo mbalimbali nchini wamekuwa wakienda katika mti huo na kubandua magome yake na kisha kuondoka nayo.
(PICHA NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na baadhi ya watumishi kabla ya kutembelea Hifadhi ya msitu wa Mazingira asilia wa Rondo pamoja na Shamba la miti la Rondo inayoosimamiwa na Wakala wa Hudum za Misitu Tanzania (TFS) ikiwa ni ziara ya kikazi katika wilaya ya Lindi mkoani Lindi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na baadhi ya watumishi mara baada ya kutembelea Hifadhi ya msitu asilia wa Rondo unaosimamiwa na Wakala wa Hudum za Misitu Tanzania (TFS) ambao mara baada ya kuhifadhiwa ambao umekuwa na wanyamapori wakali kama vile tembeo na simba ambao wamekuwa wakivamia mashamba na kujeruhi wananchi mkoani Lindi, Wa kwanza ni Mkuu wa HIfadhi ya Rondo, Richard Tarimo


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na baadhi ya watumishi wakati alipofika katika eneo ambalo tembo wanaotokea katika Hifadhi ya Mazingira asilia ya Msitu wa Rondo ambao wamekuwa wakivunja miti iliyopandwa kwenye shamba Rondo ambao baadhi ya miti hiyo imeshindwa kukua ipasavyo baada miti hiyo kuvunjwa mara kwa mara
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akisalimiana baadhi ya watumishi wakati alipofika katika ofis za Hifadhi ya Mazingira asilia ya Msitu na Msitu wa Kupandwa wa Rondo ambapo amewaagiza watumishi wa Rondo wafanye kazi kwa maarifa na weledi wa hali ya juu.
………………….
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameagiza kila Taasisi ya Uhifadhi nchini ihakikishe inaunda kikosi maalum cha askari wanyamapori watakaokuwa wakitumika kudhibiti wanyama wakali na waharibifu pindi wanapovamia makazi ya wananchi badala ya kutegemea kikosi kimoja p cha Askari kutoka Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU)


Agizo hilo amelitoa jana wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa Shamba la miti la Rondo ikiwa ni ziara yake ya kikazi katika mkoa wa Lindi.


Akizungumza na watumishi hao, Mhe.Kanyasu amesema kutokana na Serikali kudhibiti ujangili kwa kiasi kikubwa wanyamapori kama vile tembo, chui na simba wamekuwa wakitembea kila mahali kwa sababu hawana hofu ya kuuliwa kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma.


Amesema hali hiyo imepelekea mazao pamoja na maisha ya wananchi kuwa hatarini hasa kwa wananchi wanaoishi karibu na Hifadhi.


Amesema licha ya wanyamapori hao kuongezeka ikiwa moja ya sababu ni Serikali kuzuia kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi wanyama hao wamekuwa wakipita njia zao za asili ambazo tayari zimevamiwa na hivyo kusababisha matatizo makubwa kwa wananchi.


Kufuatia hali hiyo, Mhe.Kanyasu ameitaka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Hifadhi za Taifa( TANAPA) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) ziwe na vikosi maalum vya askari watakaotumika kukabiliana na wanyamapori hao wakati wanapovamia vijiji.


” Kwa sasa kukutana na kundi la tembo zaidi ya 500 katika miji ya Butiama, Dodoma pamoja Morogoro ni jambo la kawaida, Hatuwezi kutegemea KDU pekee lazima nguvu iongezwe” alisema Mhe.Kanyasu.Amesema TFS ihakikishe inakuwa kikosi hicho cha Askari katika Hifadhi za Mazingira Asilia ambako kuna wanyamapori wakali ma waharibifu wakiwemo tembo na viboko, simba na chui.


Amesema kwa sasa Wizara ya Maliasili na Utalii imekuwa ikipokea maombi mengi kwa siku kutoka kwa wananchi walioathiriwa na wanyamapori wakali na waharibifu.


Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu ametoa pole kwa wananchi wa Kijiji cha Rondo kufuatia kifo cha kumpoteza Mwalimu wa shule ya msingi pekee katika kijiji hicho aliyekufa baada ya kuuliwa na tembo baada ya kumpiga picha tembo aliyekuwa akihangaika kumnasua mtoto wake aliyekuwa amenaswa kwenye kichaka.


Aidha, Mhe.Kanyasu amezitaka Halmashauri nchini zinazopakana na Hifadhi zihakikishe zinaajiri askari Wanyamapori watakaokuwa wakisaidia kutoa msaada wa haraka pindi wanyamapori hao wanapovamia vijiji


Pia, Amezitaka Halmashauri ziangalie uwezekano wa kuwatumia askari wanyamapori wa vijiji (VGS) kwa kuandaa utaratibu maalum wa kuwakabidhi silaha pindi wanyamapori wanapovamia mashamba na makazi ya wananchi.


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Mgenda amesema kutokana na juhudi za uhifadhi unaofanywa na Mkoa huo umechangia wanyamapori kuongezeka na kuwa huru kutembea kila mahali


Kufuatia na hali hiyo, Mhe. amemuomba Naibu Waziri huyo ahakikishe Taasisi zake za Uhifadhi nchini zunatoa elimu kwa wananchi ili waweze kujihami wakati wanyamapori hao wanavamia mali na makazi yao.