Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi
Mhandisi Godfrey Kasekenya, akizungumza na wakazi wa kata ya Mutukula
wilayani Misenyi mkoa wa Kagera, wakati akikagua barabara ya mpya ya
Mutukula hadi Minziro, mpakani mwa Tanzania na Uganda.
Wakazi wa kata ya Mutukula wilayani
Misenyi mkoa wa Kagera, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi
Mhandisi Godfrey Kasekenya (hayupo pichani), aliposimama kuzungumza nao
wakati akikagua barabara ya mpya ya Mutukula hadi Minziro, mpakani mwa
Tanzania na Uganda.
Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid
Mohamed, akielezea jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi
Godfrey Kasekenya (wa pili kushoto), wakati Naibu Waziri huyo akikagua
barabara ya Omurushaka, Kyerwa hadi Murongo (KM110), iliyotengewa fedha
na Serikali kwa ajili ya kuanza kujengwa kilometa 50 kwa kiwango cha
lami.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi
Mhandisi Godfrey Kasekenya (wa pili kulia) akimsikiliza mtaalamu wa
vipimo vya ugonjwa wa COVID katika mpaka wa Tanzania na Uganda eneo la
Murongo, aliposimama wakati akikagua barabara ya Omurushaka, Kyerwa hadi
Murongo (KM 110), iliyotengewa fedha na Serikali kwa ajili ya kuanza
kujengwa Kilometa 50 kwa kiwango cha lami.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Kyaka hadi Bugene (KM60), mkoani Kagera.
PICHA NA WUU