Ndege 80 kutoka Urusi zimewasili nchini Uturuki tangia kuondolewa kwa agizo la kufunga mipaka kutokana na covid-19.
Ndege 80 kutoka nchini Urusi zikiwa na watalii zimewasili nchini Uturuki ndani ya siku baada ya kuondolewa kwa agizo la kufunga mipaka lililotangazwa na serikali kama moa ya hatua za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.
Watalii wengi kutoka nchini Urusi wameingia mkoani Antalya, mkoa mmoja miongoni mwa mikoa ya Uturuki ambayo huwa na idadi kubwa ya watalii katika msimu wa likizo ya kiangazi.
Eneo la Kusini mwa Uturuki katika fukwe za bahari ya Mediterania huwavutia watalii kwa mandhari yake ya kijani kibichi.
Kulingana na takwimu zilizotolewa na uongozi wa mikoa kuhusu utamaduni na utalii Antalya, ni watu zaidi ya milioni 5, 5 wametemebelea mkoa huo ni watalii kutoka nchini Urusi.
Safari za ndege kati ya Uturuki na Urusi zilisitishwa Machi kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.
Watu 23,000 kutoka Urusi wameingia Uturuki baada ya safari hizo kuanza upya.