Operesheni kali yakusaka wanaozidisha abiria kwenye magari ya daladala na wanafunzi kuanza arusha

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiongea na baadhi askari wa jeshi la polisi
Baadhi ya askari Polisi wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Arusha
…………………….
Na Woinde Shizza  ,Arusha
MAGARI ya abiria na  wanafunzi   mkoa ni  Arusha wametakiwa kupakia abiria kwa mujibu Wa sheria za usalama barabarani kwa kuzingatia  idadi inayokubalika kwa mujibu Wa sheria za nchi yetu .
Aidha pia ukaguzi maalumu Wa magari yote ya shule mabasi ,pamoja na vingine kama yanasifa ya kubeba abiria au sio na kama hayana sifa basi yasifanye biashara na operasheni hiyo utafanyiaka kwa Sikh 14 ili kuwathibiti na kuondoa magari yote mabovu
Mkuu Wa mkoa Wa Arusha  Mrisho Gambo ameyasema hayo leo wakati akiongea na baadhi  askari Wa jeshi LA Polisi mkoa Wa Arusha  katika ukumbi Wa Polisi mess, jiji hapa 
Alisema kuwa anataka apelekewe taarifa ya idadi ya magari yote ambayo yanakaguliwa kwa kila Siku na kwa mujibu Wa sheria za nchi pamoja na usalama barabarani ,na namna pekee ya kumuadhibu mtu ni  kwa kufuata sheria  na mtu akifuata sheria ataheshimika .
“Kwa upande Wa pikipiki kwakuwa pikipiki zimesajiliwa nataka kujua kunavituo vingapi vya kupaki pikipiki,na taxi na vituo vyote vujulikane na watu wato wajulikane na hili litasaidia kupunguza uhalifu Wa kuibiwa kwa abiria nanapenda kusema mtu akiibiwa na vituo knajulikana sisi tutadili na hicho kituo ambacho abiria amechukuwa pikipiki na kuibiwa ” alisema Gambo
Alibainisha kuwa kwakufanya hivyo itasaidia hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi Wa serikali za mtaa kwani itakupunguza uhalifu.
“Pia kumekuwa na wezi wadogowadogo (vibaka) ambao wanasumbua sana, sasa nasema tunaanzisha operesheni ya vibaka hawa kwa kweli tutaenda mitaani tutachunguza mtu akishukiwa tutamkamata tutakuja kumuuliza kwanini anashukiwa na anabanwa adi aseme hii itasaidia kukimbiza hawa vibaka maana wengi ya vibaka hawa  wanatoka nje ya mkoa huu” alisema  Gambo
Aidha alitumia muda huo kuwataka askari wa Jeshi la Polisi  kuhakikisha magari yote ya watalii hayabebi vitu vya magendo ,pamoja na vitu vyovyote ambavyo vinaenda kinyume na sheria za nchi.
Alisema kuwa kufuatia vituo vya ukaguzi wa magari ya utalii vilivyojegwa, wapo watu ambao watatumia kinyume na sheria kwani kitendo cha kutokaguliwa njiani  wengine wanaweza kutumia kama fursa ya kubeba madawa ya kulivya na kutumia vingine kinyume cha sheria.
Alitaja baadhi ya vitu ambavyo wataviangalia wakati wa ukaguzi huo ni pamoja na bima,madeni yanayodaiwa na serikali,matairi,taa,ulevi pamoja na makosa mengine mbalimbali.
Pia aliwataka wawakague madereva hao kama wanaleseni na pia wachunguze namna  namna gani madereva hao wamezipata leseni hizo.
Aliwataka askari Polisi hao kufuata sheria na kanuni zilizowekwa na kubainisha kuwa hata mfumbia macho mtu yeyote au askari yoyote Wa usalama barabarani atakaekiuka sheria ,na yoyote yule ambae atawajali watalii,huku akiwataka jeshi la polisi  kupitia kitengo cha usalama barabarani kuendelea kukazia sheria za usalama barabarani ili kuendelea kupunguza ajali za barabarani.
Pia walitumia kikao hicho kutoa zawadi kwa askari ambao walifanikisha zoezi LA ukamataji madini  ambapo walifanikisha kukamata madini yenye thamani milioni 954 yaliokuwa yakitoroshewa nchi za nje.