Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako akimkaidhi tuzo Mkuu wa kitengo cha
Ulinzi, Usalama na Mwendelezo wa Biashara wa Benki ya CRDB, Misana
Mutani wakati Benki ya CRDB ikitunukiwa tuzo tatu ambazo ni mshindi wa
kwanza katika kundi la benki na taasisi za fedha katika utekelezaji wa
sera za Osha, Tuzo nyingine ni ya ufanisi katika utoaji huduma bora
unaozingatia afya na usalama wa kazi kwa benki na ile ya kamati bora ya
Osha katika huduma za kibenki, wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku
ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi Duniani ambayo kitaifa yalifanyika
mkoani Morogoro.
“Naipongeza taasisi hii kubwa ya fedha nchini kwa kuwa mfano katika kuzingatia suala zima la usalama mahali pa kazi. Napenda kuchukua nafasi hii kuzitaka taasisi nyingine nazo kuiga mfano huu ili kuimarisha usalama na afya mahali pa kazi kwa wafanyakazi wao,” alisema Bi Khadija.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako aliyekuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo alisema serikali inatambua na kuthamini usalama na afya mahali pa kazi.
“Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua usalama na afya mahali pa kazi ni haki ya msingi ya kila mfanyakazi nchini na ndiyo sababu Rais amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha nguvukazi ya taifa inalindwa,” alisema Profesa Ndalichako.
Aidha aliwapongeza wadau walioshiriki maadhimisho hayo ikiwemo Benki ya CRDB na kuwataka kuongeza usimamizi wa usalama na afya mahali pa kazi kwenye taasisi zao.
Mkuu wa kitengo cha Ulinzi, Usalama na Mwendelezo wa Biashara wa Benki ya CRDB, Misana Mutani alisema ufanisi mzuri wa benki hiyo ndiyo uliozaa matunda ya wao kupewa tuzo tatu katika kuzingatia afya na usalama mahali pa kazi kwa wafanyakazi.
Mutani alisema fedha zilizokusanywa zimewezesha upasuaji wa watoto waliotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), kuwatibu wanawake waliokuwa na fistula waliotibiwa katika Hospitali ya CCBRT na kujenga kituo cha huduma kwa njia za simu “Call Center” katika Hospitali ya Ocean Road Ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi kwa mgojwa kupata huduma bila kulazimika kusafiri kuja kupata taarifa.
Naye Meneja na Usaidizi wa Huduma wa CRDB, Elia Mnonjela alisema wakati anaongea na wadau waliotembelea banda lao katika maonyesho hayo wamefahamishwa kuhusu huduma nafuu zinazowapa fursa ya kujikwamua kiuchumi.
“Tunayahudumia makundi yote yaani wafanyakazi na wafanyabiashara. Kwa unafuu uliopo, wafanyakazi wana wigo mpana zaidi wa kukopa katika benki yetu na kukuza uchumi wao kwa riba nafuu tofauti na awali,” alisema Mnonjela.
Kwenye maadhimisho hayo Benki ya CRDB ilitunukiwa tuzo tatu. Ya kwanza ni mshindi wa kwanza katika kundi la benki na taasisi za fedha katika utekelezaji wa sera za Osha. Tuzo nyingine ni ya ufanisi katika utoaji huduma bora unaozingatia afya na usalama wa kazi kwa benki na ile ya kamati bora ya Osha katika huduma za kibenki.