Maria Sakware, mkazi wa mkoa wa Manyara, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa fimbo na mume wake aitwae Petro Fabiano na kumsababishia majeraha katika mguu wa kushoto na kumvunja mkono wa kushoto kwa kumtuhumu kuwa amechukua elfu 10.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara ACP Benjamin Kuzaga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Timu ya makachero baada ya kufuatilia kiini cha tukio hili ilibainika kuwa huyu mume alikuwa akimpiga kwavmadai kwamba haoni shilingi elfu kumi kwahiyo akiwa anamtuhumu kwamba amemchukulia, ndiyo kilichokuwa chanzo cha kipigo hadi kupelekea kufa,” amesema kamanda Kuzaga
Aidha Kamanda Kuzaga, amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pindi wanapowabaini wahalifu na siyo kushirikiana nao.