Baadhi ya pikipiki zitakazotumika katika mapokezi na kuongoza misafara ya viongozi,Wakuu wa Nchi na Serikali watakaohudhuria mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea Jijini Dar es Salaam zikiwa tayari kwa mapokezi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi akiwa anajaribu moja ya pikipiki mpya zinazoandaliwa kwa ajili ya mapokezi na kuongoza misafara ya viongozi,Wakuu wa Nchi na Serikali watakaohudhuria mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Afisa Usafirishaji – IKULU Zuberi Kachingwa.
Prof. Kabudi akiwa anafurahia mojawapo ya pikipiki mpya zinazoandaliwa kwa ajili ya mapokezi na kuongoza misafara ya viongozi,Wakuu wa Nchi na Serikali watakaohudhuria mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea Jijini Dar es Salaam,Tanzania. Anayeshuhudia ni Afisa Usafirishaji – IKULU Zuberi Kachingwa.
Prof. Kabudi akiwa anashuhudia namna mojawapo ya pikipiki mpya zinazoandaliwa kwa ajili ya mapokezi na kuongoza misafara ya viongozi,Wakuu wa Nchi na Serikali watakaohudhuria mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea Jijini Dar es Salaam,Tanzania ikiunganishwa. Anayeshuhudia ni Afisa Usafirishaji – IKULU Zuberi Kachingwa.
Prof. Kabudi akiwa anasalimiana na Balozi Mteule wa Denmark hapa Nchini, Mette Norgaard Dissing-Spandet alipofika katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukabidhi nakala za hati za utambulisho.
Balozi Mteule wa Denmark hapa Nchini, Mette Norgaard Dissing-Spandet akiwatambulisha kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi baadhi ya maafisa aliongozana nao,wakati alipofika katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukabidhi nakala za hati za utambulisho.
Prof. Kabudi akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Denmark hapa Nchini, Mette Norgaard Dissing-Spandet. Walioko pembeni ni baadhi ya wakurugenzi na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania.
Balozi Mteule wa Denmark hapa Nchini, Mette Norgaard Dissing-Spandet akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi nakala za hati za utambulisho. Tukio hilo limefanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.
Prof. Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Denmark hapa Nchini, Mette Norgaard Dissing-Spandet pamoja na Wakurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Bw Jestas Nyamanga na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania.
Prof. Palamagamba John Kabudi na mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Jestas Nyamanga wakipunga mkono kuagana na Balozi Mteule wa Denmark hapa Nchini, Mette Norgaard Dissing-Spandet