Promosheni ya tigo kandanda yazinduliwa rasmi, washindi kujizolea mamilioni

 Na Mwandishi Wetu

Kampuni inayoongoza kwa maisha ya dijitali nchini Tanzania, Tigo, leo imezindua shindano la Tigo Kandanda.

Washindi wa shindano hili, watakuwa wakipatikana kwa kujibu maswali mbalimbali ya mchezo wa soka kupitia ujumbe mfupi wa maneno na watajishindia zaidi ya sh. Milioni 18.

Wateja watakaokuwa wakiju maswali zaidi, ndio watajiongezea nafasi ya kushinda katika shindano hilo.


Akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari, Mtaalum wa Huduma za Ziada wa Tigo, Nurdin Lugembe alisema, “Kwa miaka mingi tumekuwa tukitafuta njia ambazo wateja wetu wanaweza kushirikiana na Tigo kwa faida ya kuingiza kipato.


“Tigo Kandanda inaingia sokoni kama huduma mpya ya ubunifu ambayo itawapa wateja wa Tigo muda wa ziada kutumia simu zao kwa lengo la kujipatia pesa,”.

“Mwaliko utatumwa kupitia sms kwa mteja wa Tigo, ambaye ataweza kuanza kucheza kwa kujibu maswali moja kwa moja yanayohusu mchezo wa soka,”.


 “Washindi watakuwa wakijishindia zawadi kuanzia sh 100,000 hadi milioni 18, simu za mkononi na vocha za kufanya manunuzi katika duka la nguo la Shafii Dauda. ” alielezea Lugembe.


Balozi wa kampeni ya Tigo Kandanda, Shaffih Dauda alisema, “Ni furaha kwangu kuchaguliwa kuwa balozi wa Tigo Kandanda, wateja wa Tigo wanatarajiwa kuanza kujishindia zawadi mbalimbali kwa kupitia shindano hili.


“Baadhi ya washindi pia watajishindia vocha kwa ajili ya kufanya manunuzi katika duka langu la vifaa vya michezo,” alisema.