Raia watatu wa marekani wauawa kenya….pentagon yasema tukio hilo halina uhusiano na mzozo wa iran

Wafanyakazi
watatu wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani wameuawa kwenye shambulizi la
kigaidi katika kambi ya kijeshi ya Manda ilioko mjini Lamu 

 Wafanyakazi
2 pamoja na makandarasi wawili wameripotiwa kuachwa na majeraha mabaya
kufuatia shambulizi hilo la Jumapili, Januari 5. Wakati wa shambulizi hilo la kigaidi katika kambi ya kijeshi ya Manda,
wafanyakazi wa wizara ya ulinzi ya Marekani waliuawa, huku wengine
wawili wakijeruhiwa vibaya ila hawako katika hali mbaya,”Sehemu ya
taarifa ya ubalozi wa Marekani ilisoma. 

 
Aidha, Marekani imeapa kupambana vilivyo na magaidi wa al- Shabaab hasa wale waliotekeleza shambulizi la Manda. 
Hata hivyo, imesema tukio hilo halina uhusiano wowote na mzozo unaoendelea kati yake na Iran 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *