Rais magufuli atangaza kuwasamehe january makamba na william ngeleja kwa kumtukana kwenye simu

Rais
Magufuli amesema amewasamehe Mbunge wa Bumbuli, January Makamba na
Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja kwa kumtukana kwenye simu.

Akizungumza
leo na wataalamu wa ujenzi nchini, Rais Magufuli amesema sauti hizo kwa
zaidi ya asilimia 100  zilikuwa za kweli na alipofikilia kama suala
hilo litakwenda katika kamati ya maadili ya CCM  hali ingekuwa mbaya
kwao.

“Nakumbuka
hivi karibuni kuna watu walinitukana na nikapata uhakika kwamba sauti
zile ni zao, nikafikiria nikasema hawa wakipelekwa kwenye kamati ya
siasa adhabu itakuwa kubwa. Walinitukana kwenye simu na nikahakikisha ni
kweli ni sauti zao lakini nimewasmaehe

“Lakini
wakajitokeza wawili wakaniomba msamaha nikasema nisipowasamehe nitabaki
na maumivu makubwa sana watu hao ni January Makamba na Wiliam Ngeleja
nikaona niwasamehe tu.

“Waliomba
msamaha nikasema ni vijana  na nimewasamehe. Kama palikuwa na mambo
mambo mabaya nyuma tuyasahau ili tukaanze upya maana kusamehe siyo jambo
rahisi lakini saa nyingine inabidi usamehe,,” amesema Rais Magufuli. 
Rais
Magufuli alikuwa anazungumza katika mkutano wa siku mbili ulioanza leo
Dar es Salaam unaohusisha Bodi ya usajili wa Makandarasi (CRB), Bodi ya
Usajili wa Wahandisi (ERB),  Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na
Wakadiriaji Majenzi (AQRB).