Rais magufuli kumpokea rais wa jamhuri ya uganda mhe. yoel kaguta museven

Nchi
yetu imepata heshima ya kupokea ugeni wa Mhe. Yoel Kaguta Museven Rais
wa Uganda ambaye anatarajiwa kufika hapa nchini siku ya Alhamisi ya
tarehe 05/09/2019 kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia
tarehe 05/09/2019 hadi 07/09/2019.
 
Mhe.
Yoel Kaguta Mseven atapokelewa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere International Airport Terminal I na mwenyeji wake hapa
nchini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
muda wa saa 12.00 jioni.
 
Mhe.
Rais Museveni anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Kongamano baina ya
wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda. Aidha, Mhe. Rais Museveni
anatarajia kuzindua rasmi jengo jipya la Mfuko wa Mwalimu Julius Nyerere
lililopo katika Barabara ya Sokoine/Morogoro Dar es Salaam tarehe 6
Septemba, 2019.

Mgeni
wetu anatarajiwa kuondoka hapa nchini tarehe 07/09/2019 na
atasindikizwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Tunaomba
radhi kwamba njia atakazopitia mgeni wetu zitakuwa zinafungwa kwa muda
ili kupitisha misafara ya viongozi wetu wakuu watakaoelekea Uwanja wa
Ndege wa Mwl. J. K. Nyerere kumpokea Mgeni wetu hususani barabara ya
Nyerere mpaka Mgeni wetu atakapokuwa amewasili na siku ya kuondoka.

Kwa
kutambua ugeni huu sisi kama wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwa niaba
ya wananchi wote wa Tanzania tunamkaribisha mgeni wetu na ajisikie kuwa
yuko nyumbani muda wote atakapokuwa hapa jijini.
 
Asanteni sana.
*IMEANDALIWA NA OFISI YA MKUU WA MKOA
DAR ES SALAAM