Na Magesa Magesa,Arusha
Aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na Sekretarieti ya mkoa huo mara baada ya kuwasili Mkoani hapa na kukabidhiwa ofisi rasmi.
Katibu Tawala huyo anakuja Mkoani Arusha kuchukua nafasi ya aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa huo, Dkt.Athumani Kihamia ambaye atapangiwa kazi
nyingine na mamlaka za uteuzi.
Alisema kuwa hakuna kitu kizuri kama kufanya kazi kwa ushirikiano na umoja na kuahidi kutoa ushirikiano kwa kila mmoja bila kujali ni wa kada ya chini.
Kwa upande wake aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa huo,Dkt.Athuman Kihamia alimkaribisha katibu Tawala huyo mpya na kuhahidi yuko tayari kumpa ushirikiano pale atakapohitajika,
Kadhalika aliwashuru wafanyakazi wote wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote alichokuwepo Mkoani hapo na kuwataka kumpa katibu Tawala mpya ushirikino kama waliompatia yeye au zaidi.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa Mkoa wa Arusha,Sylivia Mamkwe alisema kuwa Kihamia anaodoka Mkoani hapa ila watamkumbuka wa utendaji kazi
wake uliotukuka.
“Dkt. Kihamia alikuwa akiwajali sana wafanyakazi hususani wa kada za chini na hakusita hata wakati mmoja kumchukulia hatua mkuu wa idara atakayebainika kumnyanyasa mfanyakazi wa kada ya chini.”Alisema Mamkwe
Maelezo ya picha,Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Dkt.Athuman Kihamia (kushoto) akimkabidhi nyaraka Katibu tawala mpya wa Mkoa huo,Misire Albano Musa(Kulia)wakati wa makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha jana(Picha na