Rc gambo aibuka juu ya taarifa dalili za ugonjwa corona arusha

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amekanusha taarifa ambazo zinaenea kwa kasi katika mitandao ya kijamii kuwa kuna mtalii mmoja raia wa China amewekwa chini ya ulinzi kutokana na kuwa na dalili za ugonjwa wa Corona .

Adai kuwa taarifa hizo ambazo zinadai kuwa mtalii huyo yupo katika katika hotali moja jina limehifadhiwa  iliyopo eneo la  wilayani Arumeru si za kweli .

Gambo amesema taarifa hizo zinazoenea katika mitandao ya jamii sio kweli na hakuna mgeni yeyote katika hotel ya hiyo kutoka China wala Bara la Asia  kama tetesi zinavyosema.

Pia Gambo amewatoa hofu wakazi wa mkoa wa Arusha kuwa wizara ya afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imejipanga ipasavyo katika kuhakikisha kuwa hakuna raia yeyote mwenye dalili ya virusi hivyo kuvuka mipaka ya nchini.