Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko |
Na Mwandishi Wetu, Katavi
Wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule zote za Sekondari Mkoa wa Katavi wametakiwa kuwa shuleni baada ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko kuondoa vigezo vya kujiunga kwa baadhi ya Shule kutoka na Mazingira.
Baadhi ya shule zimekuwa zikiagiza katika fomu za kujiunga kidato cha kwanza mwanafunzi kuripoti shuleni akiwa na panga,kwanja la kufyeka majani,rimu na mahitaji mengine kwa ajili ya usafi na kujifunzia.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua ametoa ruhusa hiyo kwa mwanafunzi yoyote aliyechaguliwa kujinga kidato cha kwanza kuripo shule hata kama bado wazazi wake hawajamnunulia sare za shule kuanza masomo na mambo mengine yatatekelezwa akiwa darasani anasoma.
Aidha amewaasa wanafunzi wote kuzingatia masomo wawapo darasani na kwa upande wa wasichana wasikubali kurubuniwa na kujiingiza katika vishawishi vitakavyopelekea kuacha masomo na kupoteza ndoto zao.
”
Afisa Elimu Mkoa wa Katavi Dr.Baganda Elpidius akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kabungu iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi |
Kwa upande wa wanaume niwatake msome kwa bidii na kuacha kwenda kwenye vijiwe vya mitaani pamoja na kutazama video zinazoonyeshwa katika mabanda zisizo na maadili muache kukimbilia maisha kwa kusema nitakuwa bodaboda japo ni kazi lakini zina muda wake wakati huu ni wakusoma kwanza”aliwaasa.