Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akikagua Maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Kawalyowa iliyopo Kata ya Ilembo Manispaa ya Mpanda ambapo amewaagiza Wakurugenzi kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati na Halmashauri itakayo shindwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake |
Na Mwandishi Wetu, Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewaagiza Wakurugenzi wote wa Halmashauri zilizopo katika Mkoa wa Katavi kuhakikisha fedha zilizopo kwenye Halmashauri zao za miradi ya Maendeleo zinatumika kukamilisha miradi husika kabla ya mwaka mpya wa fedha 2022/2023 kuanza na Halmashauri itakayo sababisha fedha kurudishwa hazina itachukuliwa hatua.
Maagizo hayo ameyatoa alipokuwa kwenye ziara ya kukagua Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Kawalyowa inayojengwa ili kupunguza msongamano wa wanafunzi kwenye Sekondari ya Kata ya Ilembo .
Amesema kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi na miradi yote ambayo imepata fedha katika mwaka wa fedha 2021/ 2022 haitakiwa kuvuka na fedha za miradi na kwa maana hiyo miradi ambayo inamaelekezo mahususi kama vile miradi ya fedha za IMF inatakiwa iwe imekamilika.
Amebainisha miradi yote ya Shule mpya za Sekondari za Kata inatakiwa kukamilika Mei 31,2022 lakini miradi mingine yote ambayo haina maelekezo maalumu inatakiwa kabla ya Juni 30,2022 iwe imekamilika .
Amesisiza kuwa maelekezo hayo yatekelezwe katika Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi na aliwataka Wakuu wa Wilaya kusimamia maagizo hayo na hataki Halmashauri yoyote kuvuka na fedha za miradi kwani wananchi wanayo mahitaji ya miradi inayotekelezwa kupitia fedha hizo.
Aidha amesisitiza kuwa hata mvumilia Mkurugenzi yoyote yule atakae chelewesha Ujenzi wa miradi anataka kuona miradi inakamilika kwa wakati ili kutimiza adhima ya Serikali ya kuwasogezea wananchi huduma karibu ili wapate huduma kwa haraka.
Pia alisema hata sita kumchukulia hatua Mkurugenzi yoyote wa Halmashauri ambae Halmashauri yake itafanya uzembe katika usimamizi na matumizi ya fedha za miradi na kushindwa kukamilisha miradi kwa wakati na fedha kurudi Hazina .
Aidha Mrindoko aliwaondoa wasiwasi wananchi wa Mkoa wa Katavi kutokana na sintofahamu baada ya kutokea mauwaji ya mtu mmoja hivi karibuni kuwa kuna mpango umepangwa wakufanya mauwaji ya watu ndani ya Mkoa wa Katavi jambo hilo halina ukweli wowote.
Hivyo amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Katavi kuwa Mkoa upo salama na wananchi waendelea kufanya kazi zao kama kawaida anaekwenda shambani aende kama kawaida na anaefanya biashara afanye bila mashaka kwani Mkoa upo salama na shwari.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Deodatus Kangu alisema kuwa wamepokea maelekezo ya Mkuu wa Mkoa watayatekeleza kama walivyo agizwa na Mkuu wa Mkoa Mwanamvua Mrindoko.
Alisema miradi yote inayotekelezwa kwenye Halmashauri watahakikisha inakamika kabla ya June 30 mwaka huu kama ilivyo ilekezwa