Rc makonda akabidhi muswaada wa mapendekezo ya sheria ya mirathi wizarani dodoma

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda  September 03 ametimiza
ndoto za Wajane kwa kukabidhi Muswada wa Mapendekezo ya Mabadiliko ya
Sheria ya Mirathi kwa Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Augustine
Mahiga kwaajili ya Kufanyiwa maboresho na kufikishwa Bungeni.

 

Akikabidhi
Muswada huo jana  Mjini Dodoma RC Makonda amesema ndani ya Muswada huo
ameainisha mapendekezo ya kubadilishwa kwa Sheria kandamizi ambazo
zimekuwa mwiba na Mateso kwa Wajane kwa muda wa miaka mingi.
Aidha
RC Makonda amesema Miongoni mwa Sheria kandamizi anazopendekeza
zifanyiwe mabadiliko ni Sheria ya Kiserikali ya Mirathi ya Mwaka 1865,
Sheria ya Mirathi ya Kimila ya Mwaka 1963 na Sheria ya Mirathi ya Kidini
ya Mwaka 1963 kwakuwa zimepitwa na Wakati na zimekuwa na Mapungufu
mengi ya Kisheria.
RC
Makonda amevitaja baadhi ya vipengele anavyopendekeza vifanyiwe
maboresho ni pamoja na kipengele cha kumpa uhalali Mke wa marehemu
kushiriki katika vikao vya mgawanyo wa mali, mjane kupewa haki ya
kurithi na kusimamia mali za marehemu, Mjane kutoondolewa kwenye nyumba
wala Mali kuhamishwa, Usawa wa watoto katika kumiliki mali za marehemu
bila kujali jinsia pamoja haki ya mtoto wa nje ya Ndoa kurithi Mali.

Vifungu
vingine ambavyo RC Makonda ameeleza kuwa ni kandambizi kwa Mjane ni
pamoja na kipengele kinachoruhusu Mjane kurithiwa na kile kinachomnyima
Mwanamke haki ya kurithi ardhi ya ukoo. 
Pamoja
na hayo RC Makonda amesema chimbuko la muswada huo ni mapendekezo
yaliyotokana na Kongamano la Wajane zaidi ya 5,181 alilohitisha mwezi
April Ukumbi wa Mlimani City ambapo katika kongamano hilo alipokea Kero
na Malalamiko yaliyomlazimu kuunda kamati iliyoshirikisha Wadau na
Wataalamu mbalimbali kutoka Serikalini na Asasi za Kiraia.
Kwa
upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Augustine Mahiga
amesema kuwa alichokifanya RC Makonda kupigania haki za wajane ni
Ushujaa wa hali ya Juu na ameweka historia ya Jambo ambalo halijawahi
kufanyika ambapo amemuahidi kufanyia maboresho ya haraka na kuwasilisha
Bungeni.