Rc mongela atembelea vijiji wilayani karatu na kutatua migogoro ya ardhi

 

Na Ahmed Mahmoud 
Mkuu
wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, amefanya Mkutano wa Hadhara
na Wananchi wa kijiji cha Buger wilaya ya Karatu kwa lengo kutafuta suluhu
ya mpaka kati ya kijiji hicho  na hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.
Katika
Mkutano huo, wananchi wa kijiji cha Buger wameiomba Serikali kuridhia
mpaka wa maridhiano wa awali, uliofanywa baina ya tume ya baraza la Mawaziri na wananchi hao ili kuwawezesha kuendelea kuishi katika maeneo hayo pasipo na
mgogoro wowote.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wakati wa mkutano huo, wananchi hao wameeleza kuwa
awali Mamlaka ya Hifadhi za Taifa iliweka mipaka ya Mikaratusi na
kupakwa rangi nyekundu kama ishara ya mpaka kwa makubaliano na baadae
kuboreshwa kwa kuwekwa nguzo kubwa hakukuwa na mgorogoro,ndipo baadae
ikawekwa mipaka mingine ambayo wanasema haikushirikisha wananchi ndipo
mgogoro huo ulipozuka.
“Sisi
tuniomba Serikali kupitia wewe Mkuu wa Mkoa itukubalie kurudisha mpaka
wa awali tuliyokubalina kwasababu huu mpaka ulioleta mgogoro
umesababisha na makazi ya baadhi ya wananchi kubaki kwenye hifadhi”.
Amesema
Sambamba
na hayo, wananchi hao wameishukuru  Serikali kwa kuendelea kuwajali
pamoja na kumshukuru Mkuu wa Mkoa huo kwa kutumia hekima kubwa na
busara katika kutafuta suluhu ya mgogoro huo kwani wanaamini utaisha
salama bila kuleta mgogangano wowote.
Tunatambua
sana umuhimu wa hifadhi hii hususani katika maeneo yatu haya, hivyo
tunaishukuru sana Serikali kwa kuwa inatusikiliza na kutafuta namna bora
ya kumaliza mgogoro huu kwa njia ya makubaliano”. Amesema Emmanuel
Matay, Mkazi wa Kijiji hicho.

 

Aidha,
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella amewaeleza wananchi hao
nia njema ya Serikali ya kuweka mipaka hiyo kwa kukwepa makazi ya watu
waliokwisha kuvamia eneo la hifadhi na kuendelea na shughuli zao za
maendeleo.

Hata hivyo,
Mhe. Mongella baada ya kuwasiliza wananchi hao, ametoa siku 10 kwa
wahifadhi wa hifadhi hiyo kushirikiana na wajumbe watatu walioteuliwa
kwenye Mkutano huo kuwakilisha wananchi kufanya tathimini ya eneno hilo
na kubaini eneo la mpaka unapopaswa kuwekwa kulingana na ramani ya
hifadhi hiyo kisha kuandaa taarifa na kuiwasilisha kwa Mkuu huyo wa Mkoa
kwaajili ya kumaliza mgogoro huo kwa kuweka mipaka ya kudumu.
Awali,
kutokana na mgogoro huo ambao umedumu kwa miaka nane, umesababisha
kusimama kwa shughuli za uwekezaji wa hifadhi hiyo na kuingizia Serikali
mapato kupitia mapato yatokanayo na utalii.