Robert mugabe amepewa hadhi ya taifa na maombolezi rasmi zimbabwe

Mugabe na mkewe
Siku tatu za maombolezi ya kataifa zimeanza Zimbabwe kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa taifa hilo Robert Mugabe. Bwana Mugabe ambaye ndio rais wa kwanza wa taifa hilo aliongoza taifa hilo hadi alipopinduliwa na jeshi 2017. 

Licha
ya hilo , chama tawala Zanu- PF kimemtangaza kuwa shujaa wa kitaifa.
Licha ya kusifiwa awali kwa kupanua sekta ya afya na elimu kwa weusi
walio wengi, bwana Mugabe baadaye alitumia ghasia dhidi ya wapinzani
wake na kuongoza uchumi wa taifa hilo ulioanguka vibaya. 

Kimataifa
mpiganaji huyo wa zamani alionekana kama dikteta kufuatia hatua ya
jeshi lake kuwashambulia wapinzani wake mbali na kunyakuwa ardhi kutoka
kwa wakulima wachache weupe ili kupiga jeki umaarufu wake miongoni mwa
wapiga kura. 

Zimbabwe President Robert Mugabe (R) inspects a guard of honour during official Heroes Day commemorations held at National Heroes Acre in Zimbabwe on August 14, 2017.

Uongozi wake umezua mjadala mkubwa tangu kifo chake.
Alikuwa maarufu miongoni mwa wapiga kura wengi hata katika kipindi chake cha hivi karibuni alipong’atuliwa mamlakani. 
Aliondolewa
mamlakani alipomfuta kazi makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa
ambaye baadaye alikuwa rais wa taifa hilo na amempongeza bwana Mugabe
tangu habari za kifo chake zianze kutolewa. 
Bwana Mnangagwa alisema kwamba chama tawala Zanu -Pf kilimpatia hadhi ya shujaa wa taifa aliyohitaji. Hakuna
muda uliotangazwa kuhusu mazishi yake , huku mamlaka nchini Singapore
ikishirikina na ubalozi wa Zimbabwe kuusafarisha mwili wake nyumbani. Alikuwa akipokea matibabu nchini humo tangu mwezi Aprili.
 Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe

Je Robert Mugabe ni nani?

Mwaka 1980, Bw Mugabe alishinda uchaguzi na kuwa waziri mkuu 
Mwaka 1982 aliushutumu upinzani kwa kujaribu kupindua serikali
Maelfu ya watu waliuawa alipolituma jeshi lake lililopata mafunzo Korea Kaskizini, kuwakandamiza maadui zake 
Mwaka 1987, alibadilisha katiba ili imruhusu kuwa rais na kuongeza mamlaka yake   Uchumi ulidororeka baada ya mwaka 2000
Wakati Mugabe aliagiza kunyakua mashamba yaliomilikiwa na watu weupe yaliyokuwa kinara ya uchumi Mfumuko wa bei ulipelekea sarufi ya taifa kuwa bila thamani na hali nchini humo ikazidi kudororeka.
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2008, Mugabe alilazimika kugawanya mamlaka na kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai
Japo kulikuwa na ghasia dhidi ya wafuasi wa Bw Tsvangirai katika kampeni za uchaguzi. 
Ndoa yake na Grace Mugabe ,anayemzidi kwa maika 40, yaweza kuwa iliyomponza, Wengi walikasirishwa na Grace kuandaliwa kuwa mrithi wake
Jeshi limeonesha kumtaka Emmerson Mnangagwa aliyefutwa kazi kama makamu wa Rais na Mugabe mwezi Novemba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *