Na Qeen Lema, Arusha
Watoa huduma ya maji ngazi ya jamii(CBWSOS) 125 wamejengewa uwezo wa namna sahihi ya kukusanya mapato kwa kutumia vyombo vya kielektroniki ambapo hapo awali walikuwa wanakusanya mapato kwa njia ya stakabadhi za Serikali
Akiongea na vyombo vya habari mapema Leo meneja uratibu vyombo vya watoa huduma ya maji kwa ngazi ya jamii Bi Valentina Masanja Kutoka RUWASA alisema kuwa lengo halisi la kuwajengea uwezo ni kwa ajili ya kuwapa uzoefu waweze kutumia mfumo mpya Wa kielektroniki.
Alisema kuwa watoa huduma hizo za maji wametokea kutoka mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro,Tanga,pamoja na mkoa wa Pwani
Alisema kuwa kwa Sasa watoa huduma ngazi ya jamii wanakusanya mapato kwa kutumia stakabadhi ila kwa Sasa wanatakiwa watumie mfumo wa kielektroniki kwa kuwa ni matakwa ya Sheria
“Ni wajibu wetu kwa mujibu wa Sheria tuwajengee uwezo kwa kuwa fedha wanazokusanya ni mali ya serikali,hivyo ni muhimu kuangalia na kutafuta mbinu za kutunza mali za umma”aliongeza
Alibainisha kuwa kabla ya kutumia mfumo huo kulikuwa na changamoto mbalimbali kama upotevu wa fedha ambazo wakati mwingine hazionekani zilipo lakini kwa kutumia mfumo wa kielektoniki
Katika hatua nyingine alisema kuwa mpango huo utaanza Sasa kwa mikoa hiyo 5 mara baada ya kupata elimu hiyo ya kukusanya mapato kwa kutumia mifumo ya kielektroniki
Alisema kuwa kwa Kanda nyingine wanatarajia kwenda kuwapa mafunzo kwa Kanda ambapo napo lengo halisi ni kuhakikisha vyombo vyote vya watumia maji wanatumia mfumo huo wa kielektroniki
Aliwasihi wadau hao wa vyombo vya watumia maji ngazi ya jamii kuhakikisha kuwa kwanza wanatumia vyema elimu ambayo wameipata sanjari na kutunza mashine hizo ambazo kwa Sasa watakabidhiwa.