Samia ataka sadc kutenga fedha zaidi,wataalam kukabiliana na uharibifu wa mazingira

Na Claud Gwandu,Arusha
MAKAMU wa Rais,Samia Suluhu Hassan amezitaka nchi
wanachama wa Jumiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kutenga fedha zaidi
na wataalam wa masuala ya mazingira ili kuhifadhi mazingira na kuokoa
rasilimali ilizobarikiwa nchi hizo.

Mawaziri pamoja na Baadhi ya Washiriki wa mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Mazingira, Maliasili na Utalii kwa Nchi 16 za Jumuiya ya Wanachama wa SADC  unaojadili kuhusu Mkakati  wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi, Uchumi wa Bluu, Misitu, Utalii, Wanyamapori  pamoja na hifadhi ya Utunzaji wa Mazingira kwa Nchi Wanachama wa SADC. wakimsikilioza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokua akifungua Mkutano huo leo Octoba 25,2019 katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa AICC Jijini Arusha

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua mkutano wa
Pamoja wa Mawaziri wanaosimamia Sekta ya Mazingira, Maliasili na Utalii
kwa Nchi 16 za Jumuiya ya Wanachama wa Maendeleo ya Kusini mwa Afrika
SADC  unaojadili kuhusu Mkakati  wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia
Nchi, Uchumi wa Bluu, Misitu, Utalii, Wanyamapori  pamoja na hifadhi ya
Utunzaji wa Mazingira kwa Nchi Wanachama wa SADC. Mkutano huo
umefunguliwa leo Octoba 25,2019 katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa
AICC Jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa
katika Picha ya Pamoja na Washiriki wa mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya
Mazingira, Maliasili na Utalii kwa Nchi 16 za Jumuiya ya Wanachama wa
SADC  unaojadili kuhusu Mkakati  wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia
Nchi, Uchumi wa Bluu, Misitu, Utalii, Wanyamapori  pamoja na hifadhi ya
Utunzaji wa Mazingira kwa Nchi Wanachama wa SADC. Baada ya kufungua
Mkutano huo  leo Octoba 25,2019 katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa
AICC Jijini Arusha.  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Akifungua mkutano wa mawaziri wanaosimamia sekta za
mazingira,maliasili na utalii wa  jijini
hapa leo,Makamu wa Rais alisema kasi ya uharibifu wa mazingira ni kubwa
kuliko  jitihada zinazofanyika katika kuhifadhi
na kuokoa.
‘’ingawa nchi za SADC zimebarikiwa kuwa na rasilimali
nyingi,bado zinakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwamo uchafuzi wa
mazingira,uharibifu wa mifumo ya maisha ya viumbe wa majini,unaribifu wa
misitu,upotevu wa makazi ya wanyamapori na bioanuai hivyo jitihada za makusudi
zinapaswa kuchukuliwa kuokoa na kuhifadhi mazingira,”alisisitiza na kuongeza:
“Ni jambo la kusikitisha kuona kasi yetu ya uharibifu
wa mazingira ni kubwa kuliko jitihada tunazofanya katika kuhifadhi na kuokoa rasilimali  tulizobarikiwa.Ili tuweze kukabiliana na
changamoto hizi,sote tuna wajibu wa kulinda na kuokoa rasilimali tunaandaa
mikakati inayoendana na protocals (itifaki) na Mipangombinu  ya SADC’’
‘’Lazima tuhakikishe tunatekeleza Mipangombinu hiyo
kulingana na hali halisi za mazingira ya nchi zetu ikiwa ni pamoja na kutenga
fedha zaidi na kuwa na wataalam wa masuala ya mazingira na pia kuzingatia kutoa
elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kulinda na kuhifadhi rasilimali za mataifa
yetu.”
Alisema kuwa nchi nyingi za SADC zina mipango mizuri
ya kukabiliana na changamoto mbalimbali 
za uharibifu na uchafuzi wa mazingira lakini  mipango hiyo hubaki kwenye mafaili na kuwa ni
ya kinadharia zaidi kuliko kuzingatia uwezo wan chi kifedha na kitaalam.
Alitaka nchi wanachama wa SADC kutumia na kuzingatia
mbinu na taaluma za kienyeji  zinazoweza
kutumika kurekebisha uharibifu wa mazingira na pia kuwa na mfumo imara ya
kusimamia utekelezaji wake
Alitaja athari zilizosababishwa na mabadiliko ya
tabianchi kuwa ni pamoja na   mabadiliko ya hali ya hewa, bahari kumeza
ardhi, mabadiliko ya misimu na viwango vya mvua 
na kusababisha kuenea kwa hali ya jangwa na ukame na mafuriko ya mara
kwa mara na kuzuka kwa magonjwa ya milipuko.
Awali Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis
Kigwangwalla ambaye ndiye Mwenyekiti wa mkutano huo wa mawaziri mkutano huo
utaridhia mapendekezo yaliyowasilishwa na wataalam ambayo yanalinda maslahi ya
Jumuiya.
Dk Kigwangalla alisema kuwa mkutano huo utajikita
katika kupima utekelezaji wa Sera na Mikakati mbalimbali kuhusu
mazingira,maliasili na utalii ikiwamo Itifaki ya SADC ya uhifadhi wa
wanyamapori pamoja na utekelezaji wa Sheria na Mipango ya Kupambana na Ujangili
na programu ya SADC ya maeneo ya uhifadhi yanayovuka mipaka.
Mikakati mingine itakayojadiliwa katika mkutano huo,ni
itifaki ya SADC kuhusu usimamizi wa Misitu na Mkakati wa miisitu,itifaki ya
SADC kuhusu Maendeleo ya Utalii na itifaki ya Jumuiya hiyo ya usimamizi  wa Mazingira endelevu,mkakati wa mabadiliko
ya tabianchi na program ya kupambana na ueneaji wa jangwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *