Serikali kuwachulia hatua kali wanaokeketa wasichana tarime.

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tarime Apoo Castro Tindwa akiongea  katika maadhimisho ya siku ya wanawake
……………………………………..

Na Frankius Cleoophace Tarime
Serikali imesema kuwa itawachukulia hatua kali wazazi na walezi  pamoja na Ngariba Wilayani Tarime Mkoani Mara  ambao wanaendeleza suala la ukeketaji  jambo ambalo linasababisha Ndoa za Utotoni, Mimba za Utoto pamoja na Ukatili kuendelea kwenye Jamii.

 Hayo yamebainishwa hivi karibuni  na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Apoo Castro Tindwa katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambapo kiwilaya katika Wilaya ya Tarime yamefanyika kata ya Mbogi.

Mkurugenzi alisema kuwa suala la ukeketaji ni kosa kubwa hivyo jamii iondikane na suala la kuwakeketa wasichana.

“Mungu amewaumba wasichana jinsi  walivyo sasa mnapowakeketa mnafanya makosa makubwa na sisi kama serikali hatutafumbia macho suala hilo lazima tuchukuea hatua kali” alisema Mkurugenzi.

Akiongea kwa niaba ya Mgeni Rasmi  ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhandisi Mtemi Msafiri, Upendo Timoth ambaye ni Afisa tarafa Inchugu  alizidi kupiga viti suala la Nyumba Nthobu kuwa nao ni ukatili japo haupigiwi kelele.

Nyumba Nthobu ni ile hali ya Bibi au mwanamke kulipia mahali mwanamke mwenzake alafu kutafuta mwanaume kwa ajili ya kuzalisha mwanamke huyo ambapo watoto hao uwa ni mali ya Mama huyo aliyelipa mahali hivyo sasa kuna haja ya kupiga vita suala hilo.

Maadhimisho hayo yameweza kushirikisha Mashirika mbalimbali ambao ni wadau wa kupiga vita ukatili wa kijinsia Sister Stella Mgaya ni Mkurugenzi wa shirika la ATFGM Masanga alisema kuwa kama shirika watendelea kushirikiana na serikali ili kupiga vita ukatili wa kijinsia.

Vile vile Leah Kimaro ambaye ni mwezeshaji  kutoka shirika la Right to Play alisisitiza  wazazi kuwapunguzia majukumu watoto wa kike huku Elizabert Sangija ambaye ni katibu wa Kamati za Halmashauri akieleza Halmashauri  akidai kuwa Halmashauri inaendelea kusaidia Wanawake licha ya ukatili kuendeleakuwepo.