Serikali yafuta ada kidato cha 5 na 6, sasa ni bure

 Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba amependekeza kufutwa ada ya kidato cha tano na cha sita hatua ambayo inalenga kuwapunguzia gharama Wazazi na kuwawezesha wanafunzi wanaotoka katika familia duni kusoma.

Akiwasilisha bungeni jijini Dodoma leo Juni 14/2022 makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Serikali ya mwaka 2022/2023.Waziri wa fedha na Mipango Dk. Mwigulu amesema kwa sasa wanafunzi wa kidato cha tano ni takribani 90,825 na kidato cha sita ni 56,880 na mahitaji ya fedha ni Sh billion 10 3.

Amesema ili kuwapunguzia gharama wazazi na walezi ada kuanzia wanafunzi wa kidato cha tano na sita inafutwa,hivyo kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha sita elimu bila malipo.