Wawakilishi wa APC wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dr Jimmy Yonanzi |
wakili James Marenga akiwasilisha mapendekezo ya wadau kupitia APC na TOMN |
Na Seif Mangwangi, Dodoma
SERIKALI imepokea mapendekezo ya wadau wa habari nchini kuhusu mapendekezo ya mabadiliko ya kanuni ya sheria za maudhui mtandaoni 2021 yaliyotolewa na waziri wa habari, michezo sanaa na utamaduni.
Wakili James Marenga |
Moja ya mapendekezo ya Serikali kwenye mabadiliko ya kanuni hizo ni pamoja na kupunguza ada za leseni za maudhui mtandaoni kutoka sh. 100, 000 ya usajili hadi sh. 50,000 na ada ya mwaka kutoka shilingi milioni moja hadi laki tano kwa mwaka.
Afisa ufuatiliaji kutoka mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA Dr Philip filikunjombe akiwasilisha mapendekezo ya waziri |
Naibu Mkurugenzi Habari Maelezo akisalimu wadau katika Mkutano huo |
Wakiwasilisha mapendekezo yao katika mkutano uliofanyika leo Jijini Dodoma Arusha Press club kupitia mradi wake wa Alternative media kwa ushirikiano na umoja wa waandishi wa habari mtandaoni (TOMN), muungano wa taasisi za habari zinazofanya utetezi juu ya haki ya kupata habari nchini(CORI) kwa pamoja wameiomba Serikali kufuta kabisa ada ya mwaka kwa wanaoendesha mitandao ya kijamii.
Kwa niaba ya APC na TOMN, wakili James Marenga amesema waandishi wa habari wanaomba ada hiyo ifutwe kabisa lakini kama itakuwa ni lazima iwepo basi Serikali ianzie kwa kiwango cha 100,000, kwa wanaoanza, laki mbili(200,000) kwa mwaka wa pili na laki tatu hadi tano(300,000-500,000 kwa miaka zaidi ya mitano.
Pia aliiomba Serikali kuondoa adhabu kali ya kufunga waandishi watakao kuwa wamefanya makosa ya kimtandao na badala yake iweke adhabu itakayokuwa mbadala wa kifungo na pia kufuta faini ya milioni1 ambayo inapendekezwa na wizara.
Amesema kuifanya taaluma ya habari kuwa jinai ni makosa makubwa kwa kuwa ni haki ya kila mtu kupata habari kama inavyoelezwa kwenye katiba lakini pia mashaka ya kihabari yanaweza kutatuliwa kupitia vyombo vingine vya kimàadili.
Maboresho hayo ambayo yamewasilishwa na Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Philip Filikunjombe, ametaja Mambo muhimu Katika Marekebisho ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni, 2020 kuwa ni; Kutofautisha kati ya Utoaji wa Maudhui kama chombo cha habari na maudhui mengine.
Nyingine ni Kuondoa masharti kwa Internet Cafes, Kuainisha Aina za Leseni za Utoaji wa Maudhui Mtandaoni, Kuondoa hitaji la Leseni kwa ajili ya Simulcasting pamoja na Kuondoa zuio la Matangazo ya Kubahatisha (Online Betting, Gambling).
Ametaja kanuni zingine zinazofanyiwa marekebisho kuwa ni;Kanuni za Maudhui,Utangazaji – Redio na Televisheni, 2018, Kanuni za Miundombinu ya Utangazaji, 2018 na Kanuni za Leseni, 2018.
Mkutano huo ulifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari na teknolojia ya Habari Dkt Jimmy Yonanzi ambaye amesema maoni yaliyowasilishwa yatafanyiwa kazi na rasimu ya mabadiliko ya kanuni hizo itatolewa mapema ili iweze kuanza kutumika.