Jafary Donge, Meneja wa Sido Mkoa wa Arusha |
Shirika la kuhudumia viwanda vidogovidogo Kanda ya kaskazini linatarajia kuwakutanisha wadau mbalimbali wa viwanda,wamiliki,taasisi za Serikali, sekta binafsi,katika maonesho ya 17 ya viwanda kwa Kanda ya kaskazini.
Aidha maonesho hayo yatarajiwa kuanza rasmi October 19 hadi 25 na kuhudhuriwa na makampuni zaidi ya 199,Huku washiriki wakiwa zaidi ya 300
Akizungumza na kipindi hiki meneja wa shirika hilo mkoa wa Arusha Japhary Donge alisema kuwa Arusha ni mwenyeji wa maonesho hayo na wadau wa maonesho hayo watatokea kutoka katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro,Tanga,pamoja na Manyara
Aliongeza kuwa maonesha hayo yana madhumuni mbalimbali ambapo lengo halisi ni kuhakikisha kuwa wigo wa viwanda hapa nchini unaongezeka
Alitaja madhumuni hayo kuwa ni pamoja na kuhamasisha ubora wa bidhaa,kubadlishana uzoefu kwa wajasirimali,kutangaza shuguli zinazofanywa na Sido,kutangaza fursa za uwekezaji zinazopatikana kanda ya kaskazini
“Haya maonesho yanazunguka na Sasa sisi ndio wenyeji ambapo tunashirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha,nadhani kuwa hii ni fursa kubwa sana kwa wajasirimali kuja kujifunza,na sio wajasiriamali pekee bali hata watanzania wote tunawakaribisha”aliongeza
Aliwataka wajasirimali ambao bado ni wageni kuhakikisha kuwa wanatumia maonesho hayo kujifunza hata namna ya kuwa na bidhaa bora ambazo zina viwango Bora vinavyotakiwa.
Alihitimisha kwa kusema kwa kuwataka watanzania,wajasirimali ,kujijengea tabia ya kupenda bidhaa zinazozalisha hapa nchini,ili.kuendelea kuinua viwanda
Kauli mbiu ya maonesho hayo ni kwa pamoja tujenge viwanda kwa uchumi na ajira endelevu.