Taasisi ya teknolojia dar es salaam (dit) washinda tuzo hii kubwa jijini dodoma

 Na Mwandishi Wetu

Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imeibuka  mshindi wa jumla katika Maonesho ya Pili ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ikumbukwe kuwa maonesho haya  yalizinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa  Ijumaa ya Mei 28, 2021 katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma na kufungwa leo June 2, 2021 na  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Prof Joyce Ndalichako.

          Tuzo ya mshindi wa jumla katika Maonesho ya Pili ya Elimu na Mafunzo ya UfundiMkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam (DIT) Amani Kakana akikabidhiwa  Tuzo na Mgeni rasmi wa kilele cha Maonesho haya  ambaye ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Prof Joyce Ndalichako. 

Akizungumzia ushindi huo, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma, Amani Kakana amesema kuwa Ushindi huo ni matunda ya kazi nzuri inayofanywa na Wabunifu wa Taasisi hiyo ikichagizwa na ushirikiano mkubwa wa wadau wakiwemo Wajumbe wa Baraza, Menejimenti,  Alumni wetu na Wanajumuiya wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT).