Taasisi za dini zatakiwa kuusaidia serikali kuleta maendeleo

 
Mkurugenzi wa shirika la Recoda Mchungaji Domonick Ringo akiwa kwenye majukumu yake

Taasisi za dini zimeaswa kushirikiana kwa pamoja na serikali katika kuleta mabadiliko hususani kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa kuwa bado jamiii inakabiliwa na uitaji mkubwa 

Hayo yameelezwa na kaimu mkurugenzi jiji la Arusha,Dkt Onesmo  mandike wakati akifunga maonesho ya wakulima yaliofanyika siku chache zilizopita kwenye kanisa la T A G Calvary temple jijini Arusha ambapo yameandaliwa na kanisa hilo pamoja na shirika la RECODA

Dkt mandike alisema kuwa Taasisi za dini zina uwezo mkubwa sana wa kufanya na kuelimisha umma juu ya matumizi sahihi hasa za tenkonolijia hasa kwenye sekta ya kilimo lakini mifugo pia.

Alisema kuwa taasisi hizo kama zikitumia kofia hiyo ni lazima mabadiliko yatatokea kwa kuwa hata waumini waliopo kwenye taasisi hizo ndio walengwa katika sera mbalimbali na mikakakti ya Taifa 

“Shirika hili la RECODA limeonesha njia kubwa sana na nuru hata kwa mashirika mengine kuwa wanaweza kuwekeza kuanzia kwa wale waumini wao na kuwaandalia wataalamu ambao wataweza kuwafundisha na kisha kuwapa mbinu mbalimbali ili kufaya kazi zenye   tija”aliongeza 

Katika hatua nyingine mkurugenzi wa shirika la RECODA,Mchungaji Dominiki Ringo ambaye pia ni mkurugenzi wa idara ya maendeleo katika kanisa la T A G alisema kuwa mpango wa kanisa hilo kwa Sasa ni kufanya miradi inayotekelezeka hasa kwenye sekta ya kilimo pamoja na mifugo 

Ringo alisema kuwa wakulima hapa nchini wanazidi kuwa chini kwa sababu baadhi Yao bado wanafanya kilimo ambacho ni Cha mazoea 

Alisema kuwa hali hiyo inawafanya washindwe kufikia malengo makubwa hivyo bado wao kama wadau wamekuja na mbinu  mbadala za kuweza kusaidia jamii 

“Tukichogundua ni kuwa hata teknolojia nazo bado hazijaweza kuwafikia wakulima ipasavyo Sasa sisi tutakuja na mkakati wa kapu la uchaguzi ili mkulima azalishe sawasawa na fursa ambazo zinapatikana eneo husika.

Naye mmoja wa washiriki katika maonesho hayo Bi Epifania Kimaro alisema kuwa maonesho kama hayo hata kama ni ya kanisa yana nguvu kubwa sana katika kuleta uelewa chanya kwa kuwa yanakuja na teknolojia mbalimbali pamoja na ubunifu ambao unalenga kuinua taifa