A Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Anjelina Lutambi (aliyesimama)
akitoa ufafanuzi kwenye mkutano wa uelimishajiwa zoezi
la ukusanyaji wa takwimu za mifugo,kilimo na uvuvi katika Kijiji cha Msikii, Kata ya Muhamo,
Mkoani Singida hivi karibuni(Pichana John Mapepele).
A. Bibi Salma
Mkumbo akiuliza swali kwa wataalamu kwenye mkutano wa uelimishaji wa zoezi la
ukusanyaji wa takwimu za mifugo,kilimo na uvuvi katika Kijiji cha Msikii, Kata yaMuhamo,
Mkoani Singida hivi karibuni (Pichana John Mapepele).
A. Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa (aliyesimama) akitoa
ufafanuzi kwenye mkutano wa uelimishaji wa zoezi
la ukusanyaji wa takwimu za mifugo,kilimo na uvuvi katika Kijiji cha Msikii, Kata yaMuhamo,
Mkoani Singida hivi karibuni(Picha na John Mapepele).
Meneja
Takwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Mkoa wa Singida, Naing’oya Kipuyo(
aliyesimama) akitoa maelezo kwa katibu
Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Anjelina Lutambi (mwenye miwani) na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa
(hayupo pichani) kwenye ofisi ya Serikali ya kijiji cha Msikii, Kata yaMuhamo,
MkoaniSingidaHivikaribuni(Pichana John Mapepele).
Elibariki Musa, Mkazi wa kijiji cha Msikii, Kata ya Muhamo, Mkoani Singida akiulizwa swali kwa wataalamu (Pichana John Mapepele).
Na John Mapepele, Singida
Serikali imesema takwimu
sahihi zilizokusanywa kutoka kwenye sekta mbalimbali za kimkakati za Mifugo,
Kilimo na Uvuvi nchini zimeifanya Tanzania chini ya Uongozi wa Rais wa Awamu ya
Tano Mheshimiwa John Pombe Magufuli kuingia kwenye Nchi za Uchumi wa Kati
duniani.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na ujumbe maalum
wa kitaifa ulioongozwa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt.
Albina Chuwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Anjelina Lutambi
wakati walipokuwa wanakagua zoezi la
kitaifa ya ukusanyaji taarifa za kina za Kilimo, Mifugo,
ufugaji wa samaki Mkoani Singida ambalo
limekamilika hivi karibuni kwa
mafanikio makubwa.
“Madhumuni
makuu ya Sensa hii ni kupata taarifa muhimu za kilimo, mifugo na uvuvi
zitakazotumika katika kupanga na kutathmini utekelezaji wa mipango mbalimbali
ya maendeleo ya sekta katika taifa la Tanzania, na endapo ukusanywaji wa
takwimu utakuwa kwenye ubora unaositahili utasaidia kulifanya taifa kupea
kwenye uchumi wa juu kabisa katika kipindi kifupi kijacho” ameongeza Dkt. Chuwa
Akifafanua
amesema taarifa kwa mfano za magonjwa ya
mifugo na mazao zitaisaidia Serikali kuainisha maeneo yanayokabiliwa na
visumbufu/magonjwa ili kuchukua hatua
stahiki na kupanga mipango ya kudhibiti.Pia taarifa kuhusu uzalishaji wa mazao
zitasaidia kujua kiasi cha uzalishaji kwa maeneo husika na kuiwezesha Serikali
kupanga upatikanaji wa masoko na uwezekano wa kuanzisha viwanda vya kusindika
mazao hayo.
Aidha
amesema taarifa kuhusu upatikanaji na matumizi ya ardhi zitatumika kupanga
mipango ya matumizi bora ya ardhi vijijini
hivyo zitatumika kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji hapa nchini.
Dkt. Chuwa
ameongeza kuwa matokeo ya Sensa
ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi yanatarajiwa kuweka msingi imara wa sekta hii kwa
miaka mingi iyajo, kwa kuwa Sekta ya
Kilimo ina umuhimu mkubwa kwenye
mustakabali wa maisha ya binadamu kwa kuwa ndiyo chanzo cha chakula na
malighafi zinazohitajika katika viwanda hususani katika awamu hii inayoongozwa na
dira ya uchumi wa viwanda.
“Kutokana na umuhimu huo, na kupitia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia
ya Mwaka 2030, Sekta ya Kilimo ilipewa Lengo la Pili la Kutokomeza Njaa, Kuwa na Uhakika wa
Chakula, Lishe Bora na Kukuza Kilimo Endelevu. Aidha, lengo hilo limesisitiza
umuhimu wa kuongeza tija katika sekta ya kilimo kwa kuongeza thamani ya mazao
na pia kusisitiza matumizi bora ya ardhi na kurutubisha udongo, ili kuongeza
uwezo wa binadamu kukabiliana na kuhimili mabadiliko ya tabianchi na athari zake
yakiwemo majanga mbalimbali kama mafuriko na ukame pamoja na majanga mengine
ikiwemo ndege waharibifu” ameeleza Dkt. Chuwa
Dkt. Lutambi amesisitiza kuwa pamoja na faida za jumla ambazo mkulima
atakazozipata Sensa hii itamsaidia mtu mmoja mmoja kutatua changamoto
mbalimbali katika kilimo,mifugo na uvuvi hasa upatikanaji wa pembejeo, huduma
za ugani, upatikanaji wa masoko kwa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.
Ameongeza kuwa takwimu ni kitu cha msingi katika
kupanga maendeleo kuanzia kwenye ngazi ya kijiji hadi taifa kwa kuwa zinasaidia
kuonyesha changamoto na mafanikio na hivyo kusaidia kupata ufumbuzi wa kudumu
wa changamoto hizo.
“Ni muhimu tukafahamu kuwa takwimu sahihi za
mifugo, mazao na uvuvi zitasaidia uchangiaji
wa malighafi za viwanda vyetu hivyo kukuza uchumi wetu ambao
tunautaka wa viwanda” amesisitiza Dkt. Lutambi
Naibu Waziri wa Kilimo
Mhe. Hussein Mohamed Bashe, kwenye hotuba yake, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wadadisi wa Sensa
ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Mwaka wa Kilimo 2019/20, iliyofanyika katika
Ukumbi wa TMDA,Mwanza Julai, 25 mwaka huu alisisitiza Mwaka huu 2020, Benki ya Dunia
imeitangaza Tanzania kuwa katika kundi la nchi zenye uchumi wa kipato cha kati,
ambapo alisema Taarifa hizi zimeleta faraja kubwa kwa sekta ya kilimo kwa kuwa ndiyo iliyotoa mchango mkubwa zaidi
katika Pato la Taifa wa asilimia 26.6 mwaka 2019 na pia inatoa ajira kwa
takribani asilimia 66 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi.
“Sekta ya
kilimo ilichangia asilimia 24.3 ya mapato ya mauzo nje ya nchi mwaka 2019.
Fedha hizi kwa kiasi kikubwa zinatumika nchini katika mambo mbalimbali ikiwemo
ujenzi wa miundombinu wezeshi ya barabara, reli, maji, usambazaji umeme na
kuimarisha miundombinu ya kutolea huduma za jamii kama vile afya na Elimu kwa
lengo la kuimarisha maendeleo ya wananchi” alifafanua Dkt. Bashe
Aliongeza kuwa, kwa mujibu wa Ripoti ya Tathmini ya Umasikini Tanzania Bara
ya Mwaka 2018, sekta hii ikiendelezwa vyema ndio pekee yenye uwezo wa kuleta
maendeleo jumuishi nchini, hivyo kuna
umuhimu mkubwa wa zoezi la sensa ya mifugo, mazao na uvuvi likafanyika kwa
ubora na kwa umakini unaositahili.
Pia wakati wa tukio la uzinduzi wa mafunzo ya wadadisi wa Sensa hii,
Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Amina Msengwa
amesisitiza kuwa takwimu zina mchango mkubwa katika maandalizi na
utekelezaji wa sera na mipango, na vile vile katika kufanya maamuzi sahihi
yanayotakiwa kufikiwa kwa kutumia ushahidi stahiki (evidence based decision
making).
Amesema Sensa ya Mwaka wa Kilimo 2019/20, ni ya tano kufanyika hapa nchini tangu nchi ipate uhuru
na inafanyika kwenye
jumla ya maeneo yaliyochaguliwa ya kuhesabia 2,820 ambapo kutokana na maeneo hayo kaya 33,807 kutoka
Tanzania bara na Zanzibar.
Kwa upande wake, Meneja Takwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Mkoa wa Singida,
Naing’oya Kipuyo ameishukuru Serikali ya Mkoa wa Singida kwa kusaidia
kufanikisha zoezi hili ambalo
limefanyika kwa takribani siku 50 ambapo pia amewapongeza wananchi kwa
kutoa ushirikiano wa kutosha.
Kipuyo amesema taarifa zilizokusanywa
kwenye Sensa hii ni za kipindi cha kuanzia tarehe 1 Oktoba, 2019 hadi tarehe 30
Septemba, 2020 na kuongeza kuwa Mkoa wa Singida umekamilisha zoezi hilo kwa
maeneo yote ambapo maeneo madogo ya kuhesabia watu yaani Enumaration Areas (EA)
90 yenye kaya 1087 zilizochaguliwa kwa ajili ya kufanyiwa sensa hii zilifikiwa