Tanapa kwa kushirikiana na hifadhi ya ziwa manyara watoa elimu kwa vijiji 25

Na Queen lema
 
shirika la hifadhi la taifa (TANAPA)kwa kushirikiana na hifadhi
ya ziwa manyara limefanikiwa kutoa elimu kwa vijiji 25 kuhusiana na
masuala mbalimbali ya matumizi bora ya ardhi ikiwa ni pamoja na namna ya
kuendelea kuhifadhi na kulinda ziwa hilo.
Akiongea jana na wataalamu wa
masuala ya sayansi na mazingira ambao walitembelea hifadhi ya ziwa hilo
la manyara Bi Noelia myonga ambaye ni kamishana msaidizi wa hifadhi ya
ziwa hilo alisema kuwa elimu hiyo imetolewa kwa vipindi tofautitofauti.
kamishna alisema kuwa elimu hiyo
ilitolewa ililenga kwa vijiji vya jirani ambavyo vinazunguka hifadhi ya
ziwa hilo ambapo pia imelenga kuokoa ziwa hilo ambalo bado linaendelea
kukabiliwa na changamoto kubwa hasa ya shuguli za binadamu.
Aidha ametaja changamoto amazo
bado mpaka sasda zinakabili ziwa hilo kuwa ni pamoja na kujaa tope
ambalo linasababisha hata kina cha ziwa hilo kuendelea kupungua siku
hadi siku tofauti na hapo awali ambapo kina cha ziwa hilo kilikuwa
kirefu sana.
kamishna Noelia amedai kuwa ziwa
hilo linajaa matope kutokana na baadhi ya wanakijiji kuendelea kufanya
shuguli kama kilimo na uufugaji kwa kutegemea vyanzo vya mito hali
ambayo hufanya matope na maji yote kurudi katika ziwa hilo na kisha
kugeuka matope.
Kutokana na hali hiyo amewaoamba
wataalamu kwa kushirikiana na wizara mbalimbali kuendelea kujikita zaidi
kwenye kutoa elimu ambayo inalenga zaidi kuyatunza na kuhifadhi ziwa
hilo kwa ajili ya wanyama lakini hata vizazi vijavyo.