Tanzania kujumuishwa kati ya nchi 7 zitakazowekewa vikwazo na marekani

Serikali
ya Marekani ina mpango wa kuziongeza Nchi nyingine 7 ikiwemo Tanzania
kwenye orodha ya Nchi ambazo Raia wake wamewekewa zuio/vikwazo vya
kuingia Nchini humo ambapo Nchi nyingine kwenye hizo 7 ni Nigeria,
Sudan, Eritrea, Myanmar, Belarus na Kyrgyzstan.


Vyombo
vya habari Marekani vimeripoti kuwa baadhi ya Nchi VISA zinaweza
zisifungiwe kabisa bali zitakua ngumu kupatikana kwa masharti (za
biashara na matembezi) Maafisa wamesema bado orodha haijakamilika kwani
mpaka Jumanne Ikulu ilikuwa inajadili kuongeza Nchi nyingine 1 au 2.

Ripoti
hiyo imesema baadhi ya Nchi hizi 7 Raia wake wameongoza kwa kupitiliza
muda wa kukaa Marekani kulingana na VISA walizopewa, kwa mwaka 2018
pekee 24% ya Raia wa Eritrea walipitiliza siku za kukaa Marekani, Raia
wa Nigeria kwa asilimia 15, Sudan 12%. 

Leo
Jumatano Januari 22, 2020 kaimu balozi wa Marekani, Dk Inmi Patterson
akihojiwa na Redio Clouds amethibitisha suala hilo baada ya jana jioni
taarifa za Tanzania na nchi hizo kuwekewa vikwazo kuanza kusambaa katika
mitandao ya kijamii. 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *