Na Queen Lema, Arusha
Nchi ya Tanzania inatarajia kukabidhi uenyekiti wa jumuiya ya wazalishaji wa almasi(ADPA) kwa nchi ya Zimbabwe kwa kuwa Tanzania ilichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Baraza la mawaziri wa ADPA toka mwaka 2021
Uenyekiti huo utakabidhiwa March 2023,ambapo makabidhiano rasmi ya uenyekiti yatafanyika rasmi katika mkutano wa nane wa kawaida wa Baraza la mawaziri wa nchi zinazozalisha almasi Afrika(ADPA) utakaofanyika katika jiji la Victoria falls nchini Zimbabwe.
Hayo yameelezwa jijini Arusha Leo na waziri wa madini,Doto Biteko wakati akiongea na vyombo vya habari kuhusiana na mkutano wa tatu wa dharura wa Baraza la mawaziri wa jumuiya ya nchi za Afrika zinazozalisha Almasi.
Biteko alisema kuwa katika kipindi ambacho Tanzania ilikuwa ni mwenyekiti wa jumuiya iliweza kupata heshima kubwa kuwajibika kwa ajili maendeleo hususani katika usimamizi wa madini ya almasi.
Alisema kuwa wameweza kupitiwaupya kwa mifumo ya jumuiya hiyo ikiwemo marekebisho ya katiba,kanuni na miongozo mbalimbali ya jumuiya.
“Tulikabidhiwa uenyekiti na tunaweza kusema kuwa tumefanya makubwa sana ila tutashuhudia uteuzii wa viongozi watatu wa taasisi watakao isimamia kwa mujibu wa katiba”alisema.
Aidha Waziri Biteko aliongeza kuwa kama nchi wameweza kujifunza zaidi usimamizi wa sekta hususani kwa madini ya almasi ambapo poa nchi wanachama na hata wasio wanachama walipata nafasi ya kuja kujifunza Tanzania namna ilivyofanikiwa kuwaendeleza wachinbaji wadogo