Tanzania ya sasa chini ya rais samia suluhu hassan

 Na Mwanaidi Kipingu


Mnamo mwaka 1961 nchi yetu ya Tanzania ilipata Uhuru kutoka kwa mkoloni . Viongozi na waasisi mashuhuri waliweza kupigania Uhuru wetu, wakiongozwa Baba wa Taifa letu Mwl. Julius Kambarege Nyerere .

Nchi yetu ya Tanzania ni nchi iliyosheheni vivutio vikubwa vya kihistoria katika Bara la Afrika na Duniani kwa ujumla.
Tunajivunia nchi yetu ya Tanzania kwani nchi yenye kitovu kikubwa cha Amani, ujamaa, upendo na utulivu tangu Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar .

Katika vipindi vyote vya historia ya Uongozi wa nchi yetu ya Tanzania kuanzia kipindi cha baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere mzee wa Ruksa mzee wetu Ally Hassan Mwinyi , Hayati Benjamini William Mkapa , mzee wetu Jakaya Mrisho Kikwete , Hayati Dkt John Pombe Magufuli Taifa letu la Tanzania limeendelea kuwa kitovu na Nembo ya Amani katika bara la Afrika na Dunia.
Kipekee na dhati kabisa historia ya nchi yetu haitofutika chini ya uongozi wa mama bingwa na hodari Mh, Rais Samia Suluhu Hassan ni historia ya kipekee kabsa katika nchi yetu ya Tanzania tangu tupate Uhuru nchi yetu ya Tanzania kuwa chini ya mwanamama na mwanamke wa kwanza kuongoza Taifa letu.

Natumaini ile dhana iliyojengeka kwenye jamii kwamba mwanamke hawezi mpaka awezeshe imefika mwisho katika serikali hii ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan

Rais Samia Suluhu Hassan ameionyesha jamii kwa vitendo kwamba wanawake ni viongozi hodari , wachapakazi , wasikivu , na watendaji kweli kweli naamini kupitia Rais wetu jamii hasa yenye mfumo Dume na ukatili dhidi ya wanawake wamepata somo na kudhihirishiwa kwa vitendo chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wanawake ni Tunu na ni chachu katika maendeleo ya Taifa hili hasa wakiaminiwa na kupewa vipaumbele katika nyanja mbalimbali za kijamii mfano kisiasa, kiuchumi, na kujamii .

 Kwa kumalizia Uongozi wa Taasisi ya Jitambue Mwanamke unatambua na kuunga mkono Jitahada zote zinazofanywa na Serikali yetu chini ya mama *Samia Suluhu Hassan

#MUNGU IBARIKI AFRIKA#

#MUNGU IBARIKI TANZANIA#