Na,Swalehe Juma Matukio Daima Mwanza.
Mamlaka ya usafiri wa anga nchini (TCAA) imetoa mafunzo ya siku moja kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Ngaza pamoja na Shule ya Sekondari Nsumba Jijini Mwanza.
Yenye lengo la kuwajengea vijana hao fursa mbalimbali ambazo zinapatikana katika Mamlaka ya usafiri wa anga.
Baada ya kugundua awana uelewa wa kutosha kuhusiana na mamlaka ya usafiri huo.
Pia waweze kujua fursa mbalimbali zinazopatikana katika mamlaka hiyo ambapo mafunzo hayo yatafanyika mikoa mbalimbali ya Tanzania ikiwemo Zanzibar.