Tecno kuwa kampuni ya simu pendwa zaidi duniani

Ni  wazi hichi ni kipindi cha kufanikiwa kwenye uchumi wa utandawazi, kuanzia migahawa, magari,

viwanda vidogo na vikubwa na biashara nyingine nyingi zimekuwa zikipambana zaidi kutengeneza jina

kubwa kote duniani huku pia ikiangalia zaidi masoko ya ndani.

Ulimwengu wa biashara umeorodhesha kanuni hii kama "Glocalization", Neno hili hutumiwa kuelezea

bidhaa au huduma ambayo imeendelezwa na kusambazwa ulimwenguni kote lakini pia inarekebishwa ili

kuendana na mahitaji ya mtumiaji katika soko la ndani.

Kiasi cha watu bilioni 7.8 duniani kote wanatofautiana sana kwa upande wa mahitaji, manunuzi,

mitazamo, kufikia miundombinu, umeme na mitandao ya mawasiliano.

Uwezo wa kutambua na kutengeneza bidhaa zinazokidhi mazingirz tofauti ya watumiaji kwenye nchi

tofauti na mabara imewezesha TECNO kuuza kwa kiasi kikubwa cha bidhaa bora za simu kwenye soko la

Afrika, kusini na kusini mwa bara la Asia.

UIMARA KATIKA SOKO LA SIMU

Glocalization imewezesha TECNO kujiweka kwenye nafasi ya juu kwa kuwa na bidhaa bora za simu za

kiganjani na kuuza bidhaa nyingi barani Afrika.

Mwezi Juni mwaka huu, TECNO ilishika nafasi ya tano kwa kuwa moja ya bidhaa zinazopendwa zaidi

barani Afrika, ikiipita Apple.

Katika robo ya kwanza ya mwaka 2020, TECNO iliendelea kuwa na soko linalokuwa wakati duniani kote

usafirishaji wa simu za kiganjani ulishuka kwa asilimia 13 kutoka mwanzoni mwa mwaka huu kwa sababu

ya ugonjwa wa Corona.

Katika kipindi ambacho uuzaji wa bidhaa nyingi ulishuka kwa kiwango cha tarakimu mbili, mkakati wa

TECNO katika kutumia teknolojia ya kisasa kuendana na soko ulizidi kuimarika ili kuendelea kuuza simu

nyingi zaidi za kiganjani kama ilivyokuwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2019.

TECNO pia inafanya vizuri sana katika masoko mengine kama vile India, Pakistan, Thailand, Colombia, na

Ukraine. Kampuni imetengeneza uwepo mkubwa wa kidunia kwa zaidi ya wasambazaji 2,000 na vituo

vya huduma vya mauzo.

Kwa asili ikiwa imetengenezwa kwa ajili ya masoko ya Afrika, kwa sasa TECNO inakua na kuwa bidhaa ya

kimataifa kati ya kundi la bidhaa za simu za mkononi.

TEKNOLOJIA

Barani Afrika ambako TECNO ndo iliuza simu zake za kwanza, kampuni inatambua kuanzia mwanzoni

kabisa kuwa ili mtu aweze kupata mawasiliano kokote aendako alihitaji kuwa na laini tofauti tofauti

kulingana ili kuepuka shida ya kimtandao. Na kuwa na simu zaidi ya moja kuweka laini tofauti tofauti ni

gharama kwa watumiaji. Hivyo, TECNO ilitambua hali hii na hivyo kwa mara ya kwanza ilizindua simu ya

laini mbili mnamo mwaka 2007, ni kama miaka miwili kabla ya wapinzani wake kwenye soko.

TECNO inatambua kuwa uwepo wake mkubwa katika soko la Afrika kunaipatia kampuni hiyo uelewa ni

nini watumiaji wanahitaji kwenye simu za kiganjani.

TECNO pia inatambua mahitaji tofauti ya soko; kwa mfano lugha za nchi tofauti tofauti ziko kwenye simu

za TECNO, na hata katika kutambua na kukidhi soko la nchi ya Ethiopia kwa kuweka lugha asili ya

Amharic. Na bei za simu za TECNO ni chini ya bei za simu nyingine kwa asilimia 10.

Sifa mojawapo pekee ya simu za TECNO ni kwamba zimepewa uwezo wa kamera. Kwa kutambua

watumiaji wa simu wa Afrika simu janja hizo za TECNO zinapiga picha zenye muonekano mzuri, na hasa

kipindi cha usiku na katika mazingira yenye mwanga hafifu.

TECNO ilitengeneza simu zenye uwezo mkubwa wa camera ziitwazo CAMON ambazo zina kamera ya

mbele na nyuma inayopiga picha nzuri kwa muonekano mzuri wa ngozi na pia inatumia Artificial

Intelligence (AI) kutambua eneo la picha.

Swala la tatizo la umeme kwa nchi za Afrika liko wazi, na hivyo TECNO inatumia teknolojia ya kuwezesha

betri la simu kufanya kazi kwa muda mrefu bila kuchaji. Imetengenezwa kwa vifaa ambavyo hutumia

umeme mdogo.

Ikiwa nchi duniani zinaenda kukuza mauzo ya simu za kiganjani kutokana na kupungua kwa ugonjwa wa

Corona na kuondoa sheria ya kutotoka nje, Glocalization ni muhimu kwa bidhaa kuuzika.

Kwa mujibu wa uchambuzi uliofanywa na Mason Group, ambayo ni kampuni ya ushauri ulimwenguni

inayojikita kwenye maswala ya teknolojia ya simu, inatazamiwa kuwa mauzo ya simu za kiganjani

duniani yatakuwa makubwa kwenye masoko ya Asia Pacific na Kusini mwa Jangwa la Sahara kufikia

mwaka 2024.

“TECNO inajidhatiti kuleta simu janja bora na zenye teknolojia ya kisasa kwa watumiaji katika soko lenye

bei shindani. Kutokana na kujidhatiti huku tumekuwa tukiwekeza kwa kiasi kikubwa ili kuongeza ubunifu

kwa ajili ya wateja wetu”, Eric Mkomoye, Meneja uhusiano wa TECNO, amesema.

Kwa Mawasiliano;

Kampuni: TECNO MOBILE LIMITED

Nambari ya simu: 0717543251

Nchi: Tanzania

Barua pepe: https://www.tecno-mobile.com/tz/home/#/