Tigo tanzania washiriki kongamano la nne la tehama , watangaza fursa kwa vijana.

Kampuni inayoongoza katika kuhakikisha Mtanzania anaishi maisha ya kidijitali nchini,Tigo Tanzania ,leo wameshiriki katika kongamano linalofahamika kama “Tanzania Annual ICT Conference (TAIC)” na maudhui  ya Mkutano huo kwa Mwaka huu 2020 yamejikita sana katika huduma za Kimtandao kuelekea mapinduzi ya awamu ya nne ya viwanda “Digital transformation towards fourth Industrial revolution”   

                                                                                                  Akizungumza katika Mkutano huo mwakilishi kutoka Tigo Tanzania ambae pia Ni Mkuu wa kitengo cha huduma za kifedha biashara na mahusiano Bi. Faith Pella  ameipongeza serikali kwa juhudi kubwa inayofanya kuziunga mkono Taasisi binafsi hasa kwa upande wa huduma za Kimtandao maana  kupitia mashirika yake kama vile TANESCO, DAWASCO n.k ambapo Sasa mtu anaweza kulipia kodi , bili na madeni mbalimbali Kidigitali kupitia simu ya mkononi 

“Najivunia sana kuhusu nchi yangu na SERIKALI yangu ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu wao ndio namba moja kwenye kutangaza na kusukuma Maendeleo ya Kidigitali hapa nchini , ukiangalia huduma nyingi za kiserikali zimeunganishwa moja kwa moja na malipo kwa huduma za Kimtandao ” alisema Bi. Faith Pella.

Aidha kwa upande mwingine amesema Tigo imekua kinara katika utoaji wa fursa kwa vijana kupitia huduma zake mbalimbali na kuongezea kuwa bado nafasi zipo kwa vijana kuweza kujipatia kipato kupitia Uwakala wa Tigo Pesa na huduma nyingine mbalimbali zinazotolewa na Kampuni iyo namba moja Nchini.

Mkutano huo unaendelea kwa siku tatu Mfululizo na leo ilikua ni siku ya Pili katika Ukumbi wa JNICC uliopo Posta Jijini Dar es Salaam.