Tigo waja na bonge la ofa “cha asubuhi”.

  Na Mwandishi Wetu

Dar es Salaam, Jumanne, 15 Juni 2021 – Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidijitali, Tigo Tanzania, leo imezindua kampeni mpya ya siku 90 inayoitwa Cha Asubuhi. Katika kampeni hii mpya kila mteja anayenunua kifurushi cha kila siku, kila wiki au kila mwezi atapata bonasi ya dakika za bure kupiga Tigo kwa Tigo kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 3 asubuhi.

Mteja wa kifurushi cha kila siku atapata bonasi ya dakika 10 hadi mb 10, wakati mteja wa kifurushi cha kila wiki atapokea dakika 70 hadi mb 700 na mteja wa kifurushi cha kila mwezi atapata dakika 300 hadi GB 3.

Akizungumzia kampeni hiyo, Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa  Tigo, David Umoh, alisema, “Daima tunatafuta njia za ubunifu za kuwazawadia wateja wetu wenye kazi na kuwafurahisha, kampeni hii inatoa fursa nzuri ya kuungana na wateja wote tuliokuwa nao kwa muda mrefu. ”

“Tunaamini kuwa mipango mingi hufanywa mapema asubuhi, na kwa kuwa tuna nia ya kukidhi mahitaji ya wateja wetu kote nchini. Kampeni hii inawapa fursa watu wanaoamka mapema na wale ambao wanapendelea kupanga shughuli zao za kila siku kuanzia asubuhi. ” alisema Umoh.

“Kwa miaka mingi Tigo Tanzania imekuwa ikianzisha ubunifu kama vile Facebook ya bure kwa Kiswahili, simu mahiri za Kiswahili na vifurushi kama tulivyofanya leo.

“Mipango yetu ni kuhakikisha tunaondoa vizuizi kwa wateja wetu kwa ajili ya kufanya mawasiliano ya muhimu kupitia kampeni mpya ya Cha Asubuhi.

“Zaidi ya wateja milioni 12 wa Tigo wataweza kuamka na kupiga simu za bure, kuperuzi mtandao, bila wasiwasi wa kuwa na muda wa maongezi kwenye simu zao. Hii inadhihirisha juhudi zetu katika kuwa fursa inayowapa wateja wetu huduma bora, ” alisema Umoh.

Kampeni hiyo itaendelea kwa siku 90 na ipo kwa ajili ya wateja wote wa Tigo. 

Mteja anachotakiwa kufanya ni kununua kifurushi pendwa kupitia menyu ya USSD * 147 * 00 #, Tipo Pesa App au tavuti ya Tigo na kupata bonasi ya muda wa maongezi, bonasi ya data papo hapo, ambayo wanaweza kutumia kati ya saa 12 asubuhi hadi saa 3 asubuhi kwa kila siku bila malipo