Tiketi za kuangalia mpira sasa kulipiwa kwa tigo pesa

 Kampuni ya mawasiliano nchini Tanzania Tigo kwa kushirikiana na chuo Cha taifa Cha kuhifadhia data NIDC Leo wamezindua njia rahisi kwa washabiki na wapenzi wa Mpira kuweza kununua tiketi zao kwa njia ya simu kwa mtandao wa Tigopesa

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mkurugenzi mkuu wa kitengo Cha tigopesa Angelica Pasha alisema kuwa Tanzania ni nchi ya kuigwa kutokana na mageuzi makubwa ya kimtandao na dhamira ya Kama kampuni ya tigo  ni kuweza kuwafikia wananchi woote kwa nyanja tofauti kutokana na uhitaji wao

Naye afisa uhusiano wa chuo cha taifa Cha kuhifadhia data NIDC Geophrey Mlewa amesema kuwa ushirikiano uliofanyika utasaidia kwa kiwango kikubwa kukuza michezo nchini hasa katika mechi inayotarajiwa kufanyika dhidi ya Simba na yanga hii itawawezesha wanamichezo na washabiki wote kupata tiketi zao kwa wakati.

Hata hivyo mkurugenzi wa michezo Yusuph Singo alisema kuwa wao kama serikali jukumu lao kubwa  ni kuhakikisha wadau na wapenzi wa Soka  nchini hawapata changamoto wakati wa mechi na kuziba mianya ambayo italeta hitilafu kwenye Soka hivyo kutokana na hatua hiyo itasaidia kutatua changamoto kadha was kadha

Kwa upande wa wadau wa soka mkurugenzi wa fedha na utawala kutoka klabu ya Yanga Mfikirwa haji amewataka wadau na wapenzi wa soka kuweza kujitokeza kwa wingi kupata tiketi kwa njia ya tigo pesa na kwa njia hii itawasaidia klabu kupata mapato kwa wakati